BAADA ya Waziri wa
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), kuwashukia viongozi wa jiji kuwa
ndiyo chanzo cha kukithiri uchafu jijini, Meya wa jiji hilo Dk Didas Masaburi
amejibu kwa kusema tuhuma hizo hziwahusu.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki, na Meya huyo wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari
kuhusu kikao cha kufunga mwaka 2012.
Masaburi alisema kauli ya waziri huyo, inaonekana
kujichanganya kwani kazi ya kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi siyo ya
jiji bali wahusika wakuu ni Halmashauri.
Alisema kazi kubwa ya mamlaka ya jiji ni
kusimamamia hali ya usafi usafi wa dampo liliko Pugu Kinyamwezi.
“Hizo lawama wanapaswa wazielekeze kwenye
Halmashauri kutokana na wenyewe kushindwa kupeleka taka na siyo sisi jiji, kama
wenyewe hawatuletei taka dampo na alaumiwe”alisema.
Dk Masaburi anastajabishwa, utaratibu unaotumiwa na
baadhi ya mawaziri kwa kuzishambulia Halmashauri kuwa zinafuga uozo wa uchafuzi
wa mazingira, ambapo hata huko kwenye
ofisi za wizara zao upo uchafu.
Alitoa wito kwa Serikalli Kuu kubadili utaratibu
wake kwa kuzitengea fedha za kutosha Halmashauri hizo na kuzifikisha kwa
wakati, lengo likiwa ni kwenda sambamba
na sheria ya mazingira ya mwaka 2004.
Alisema vyanzo ya mapato wakati mwingine vinaweza
kuwa chanzo cha Halmashuri hizo kushindwa kusimamia sheria hiyo ya utunzaji wa
mazingira.
No comments:
Post a Comment