Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries, David Mgwasa (katikati) akiwa na Meneja Masoko Taifa wa kampuni hiyo, Joseph Chibehe (kushoto) na Meneja Masoko Nchi za Nje, Bavon Ndumati wakionesha kimywaji kipya cha Zanzi Cream Liqueur wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Habari Mseto Blog)
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries (TDL) wazalishaji wa bidhaa bora zaidi za vinywaji vikali na mvinyo hapa nchini, jana walizindua kinywaji kipya kiitwacho Zanzi Cream Liqueur katika uzinduzi uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Akizungumza na wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa alisema, ana uhakika kinywaji hicho kitapendwa na wengi kwani ni cha Kitanzania na kimezingatia ubora wa kiwango cha Kimataifa katika kuzalisha wake.
Mgwassa aliwataka Watanzania kujivunia kinywaji hicho na kusema TDL ikiwa ni kampuni ya kizalendo itaendelea kuhakikisha inazidi kuitangaza Tanzania kwa kuzalisha bidhaa bora zinazopendwa na wengi ndani na nje ya nchi.
“Kwetu sisi TDL tunajivunia kuzindua rasmi kinywaji cha Zanzi Cream Liqueur kwani kinazalishwa na Watanzania na kimebuniwa na wazalendo wa nchi hii, huu sasa ni wakati wa kutembea kifua mbele kujivunia kinywaji hiki na naamini kitavutia wengi kutokana na jinsi kilivyotengenezwa na kikiwa na ubora usio na shaka.”
Mgwassa alisema, nia ya kuzalisha kinywaji cha Zanzi Cream Liquer ni baada ya kuona kuna vinywaji vingi vya aina hiyo vikiingizwa nchini kutoka nje, hivyo TDL ikataka kuzalisha bidhaa bora zaidi na ya kipekee hapa duniani.
Naye Meneja Masoko Taifa wa TDL, Joseph Chibehe alisema kinywaji hicho kitapatikana katika chupa zenye ujazo wa 750ml na pakiti zenye ujazo wa 100ml, huku kikiuzwa kwa bei ambayo watu wengi wataimudu.
Chibehe alisisitiza kwamba kinywaji hicho kitapatikana kote nchini na watahakikisha kinapenya katika soko la Kimataifa, ili kuitangaza Tanzania juu ya vinywaji bora zaidi vinavyozalishwa na kampuni hiyo.
Zanzi Cream Liqueur ni kinywaji cha watu wa aina zote ingawa uzoefu unaonekana aina hiyo ya vinywaji vinapendwa zaidi na wanawake, kutokana na radha yake, humfanya mnywaji ajisikie mwenye furaha muda wote pia kikiwa na mambo mengi ya kuvutia.
No comments:
Post a Comment