HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 29, 2012

UCHAGUZI UVCCM KATA YA KAWE SASA MOTO, AMANI NKURLU NAYE AGOMBEA NAFASI YA UENYEKITI

Mgombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM kata ya Kawe Amani Nkurlu (kulia) akirudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa Katibu wa UVCCM kata ya Kawe Bi. Aisha Katundu.
Katibu wa UVCCM kata ya Kawe Bi. Aisha Katundu (kushoto) akipokea fomu aliyoijaza Bw. Amani Nkurlu kwa nafasi ya kugombea Uenyekiti UVCCM kata ya Kawe alipofika ofisini hapo leo saa 7 mchana.
Mgombea wa Uenyikiti wa UVCCM kata ya Kawe, Amani Nkurlu, akizungumza machache na Katibu wa CCM Kawe Bi. Aisha Katundu katika ofisi za CCM Kawe.
Amani Nkurlu akijaza fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM kata ya Kawe.
Baadhi ya wakereketwa wa CCM katika picha ya pamoja nje ya ofisi ya CCM Kawe. Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa tawi la Umbwelani Kawe- Ramadhani Malenge, Katibu wa Wazazi Kawe- mama Katenda, mgombea nafasi ya ukatibu UVCCM kata ya Kawe – Sambili Tegemeo na mgombea nafasi ya Uenyekiti UVCCM kata ya Kawe - Amani Nkurlu.Picha na Josephat Lukaza
Baada ya uchaguzi wa UVCCM katika kata la Kawe kuvurugika mapema mwaka huu, uchaguzi huo unaorudiwa sasa umefika patamu ikibakia siku moja tu kuchukua fomu huku vijana wengi wakijitokeza kuwania nafasi mbali mbali katika jumuiya hiyo ya vijana illiyopo wilayani Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa wagombea wa Uenyekiti wa UVCCM katika kata hiyo, Amani Nkurlu (23) alisema “Siku zote nimekuwa nikitafakari ni kwa namna gani nitaweza kutoa mchango wangu katika chama na kuchangia mustakabali wa taifa letu Tanzania kwa ujumla.”
“Ninaamini CCM bado inahitaji vijana makini na wengi zaidi wakukisemea, kuishauri na kuleta chachu ya maendeleo katika utendaji wake wa kazi wa kila siku kichama na kiserikali. Hii ndio dira yangu kwa CCM, nina imani na chama changu na nimejikita katika kuchangia mabadiliko hayo kupitia Umoja wa Vjiana,” Nkurlu alisema. 
Nkurlu ambaye ana Shahada ya Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) ameshawahi kushika nyadhifa mbali mbali za uongozi ukiwemo; Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM – Tawi maalum la Kambarage SAUT, Waziri wa Mambo ya Nje, Mbunge katika serikali ya wanafunzi, na Rais wa AIESEC akiwa hapo hapo chuoni. Mwaka 2010 Nkurlu pia alipata kugombea nafasi ya Umakamu wa Rais katika serikali ya wanafunzi chuoni hapo lakini hakufanikiwa kwa kupata kura 1278 kati ya kura 2995 zilizopigwa na 54 kuharibika.
Hivi sasa Nkurlu anamalizia Stashahada ya juu kutoka Chuo cha Diplomasia na pia ni mwajiriwa katika moja ya makampuni ya mawasiliano na matangazo jijini Dar es Salaam kama Mshauri wa Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

Pages