Na Father Kidevu Blog, Dar Es
Salaam
KAMATI ya Miss Tanzania imesema kuwa Mrembo Maggie Munthali hana pingamizi lolote katika kushiriki mashindano hayo kwa kutumia jina la Tanzania na badalaye kufanya hivyo anatumia uzalendo wake kuitangaza nchi Kimataifa.

Ufafanuzi huo umekuja
kufuatia malamiko yaliyotolewa na baadhi ya wadau wa Urembo hasa Watanzania
waishio katika jiji la Washingtoni DC, Marekani juu ya Uhali wa Mrembo Maggie
Munthali kuvaa beji ya Miss Tanzania katika mashindano ya kumsaka Miss Afrika
USA 2012.
Akizungumza na Blogu hii
Msemaji wa Kamati ya Miss Tanzania Hidan Ricco amesema kuwa Kamati ya Miss
Tanzania haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano hayo,
kwani shindano hilo linawahusu warembo waishio huko lakini wanatoka Tanzania.
Awali akitoa historia ya
Mrembo huyo, Rico alisema kuwa Kamati inamfahamu vyema mrembo Maggie Munthali
kwani aliwahi kushiriki mashindano hayo ngazi ya Vitongoji na kuishia ngazi ya
kanda.
Tumesoma
maoni yenu kupitia mitandao ya kijamii Blogs inaohusu taarifa ya mrembo Maggie
Munthali kushiriki shindano la urembo la Miss Africa USA.
“Mrembo
Maggie Munthali alishiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania Kitongoji cha
MZIZIMA mwaka 2005.” Alisema Ricco.
Pia
aliendelea kwa kusema kuwa Mrembo Maggie alikuwa miongoni wa waliofanikiwa
kuingia TOP 3 ya shindano hilo hivyo kupata nafasi ya kuwakilisha kitongoji
hicho katika ngazi ya KANDA YA ILALA kwa mwaka huo.
Mrembo
huyo hakupata nafasi ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa mwaka huo
2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.
Kanda
ya Ilala kwa mwaka huo iliwakilishwa na FEZA KESSY, Perminda Raj na LILIAN
MUSHI, na mshindi wa mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa taji la
MISS WORLD AFRICA 2005.
Ricco
amesema Kamati ya Miss Tanzania haijui ni vigezo vipi vinatumika katika
shindano hilo, na maamuzi yakumpa jina Miss Tanzania na Kamati inaamini kuwa ni
mrembo anayewakilisha Tanzania japokuwa hakuingia katika Fainali za
Taifa.
Kamati
inamtakia kila la heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza jina la
Tanzania katika fani ya urembo.
Father
Kidevu Blog ilifanikiwa kufanya utafiti juu ya washiriki wa shindano hilo na
kubaini kuwa sio Mamiss halisi wa nchi walizotoka kwani baadhi ya nchi walikuwa
zaidi ya mmoja kama vile Kenya.
Pia baadhi yao Umri unaonesha dhahiri kuwa umekwenda sana kwani
washiriki wanapoaswa kuana miaka kuanzia 18 lakini isizidi 29 na hawaendani na
vigezo halali vya mashindano ya Urembo yanayofanyika kila mwaka katika nchi
husika kwaajili ya kushiriki Miss World.
Haya
ni baadhi ya Masharti na Vigezo vya Mshiriki ambayo yapo katika mtandao huu
http://www.missafricaunitedstates.com/application/registration/
ELIGIBILITY
1.Applicant must have at least one parent from an African country.
2. An applicant with parents from two countries will choose to represent only one country of her choice.
3. Applicants must be at least 18 years old on or before the date of the pageant she wishes to compete in.
4.Applicants above 29 years of age will not be accepted
5.We accept Applications from students, professionals and girls wishing to develop themselves and improve their status.
6. Applicants are strongly encouraged to have a humanitarian platform and realistic project to uplift the community in need.
7. No Pageant Experience is required.
8. Applicants must be female at birth and never married.

No comments:
Post a Comment