Alain Traore wa mali aliyesimama akishangilia kwa staili ya kufutwa vumbi viatu pamoja na Florent Rouamba. Burkina Faso iliichapa Ethiopia mabao 4-0.
JOHANNESBURG, Afrika Kusini
NYOTA Alain Traore alifunga mara mbili dakika za 33 na 73 na
kuwawezesha wachezaji 10 wa kikosi cha Burkina Faso juzi usiku kushinda mabao 4-0
dhidi ya Ethiopia na kuhitimisha mfululizo wa mechi 18 bila ushindi katika
Mataifa Afrika.
Ushindi wa mwisho wa Burkina Faso ulipatikana mwaka 1998, lakini
juzi Traore, pamoja na Kone aliyefunga dakika ya 78 na Pitroipa dakika ya 90, walihitimisha
jinamizi hilo na kuipaisha timu yao kileleni mwa msimamo wa kundi C kwa
kufikisha pointi 4.
Mapema hiyo jana, mabingwa watetezi waliponea chupuchupu,
baada ya kusawazisha mwishoni na kuambualia sare ya 1-1 dhidi ya Nigeria,
katika mechi ambayo kiungo John Obi Mikel alikosa penati, huku kipa Kenedy
Mweene akisawazishia Zambia kwa njia hiyo.
Kocha wa Burkina Faso, Mbelgiji Paul Put, alifurahishwa na
matokeo ya mechi yao, yaliyowaweka juu ya kundi hilo linalojumuisha pia timu za
Zambia, Nigeria na Ethiopia, ambapo sasa Burkina itamaliza na Zambia, huku
Nigeria ikilaruana na Ethiopia hapo Jumanne Januari 29.
No comments:
Post a Comment