Makao Mkuu ya NCCR-MAGEUZI
Mbunge wa Kasuru, Moses Machali (katikati) akizungumza kabla ya kukabidhi kadi ya uanachama kwa mwanachama mpya aliyejiunga na chama hicho.
Eddo Makata akizungumza na waandishi wa habari baada ya kujiunga na NCCR-MAGEUZI.
DAR ES SALAAM. Tanzania
BAADA Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kumtimuwa uwanachama Edo Mwamalala, hatimaye
mwanachama huyo ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mageuzi ya Taifa (NCCR-
Mageuzi).
Akizungumza na wandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwamalala, alisema harakati za kisiasa
alizianza tangu akiwa kijana, kuwa muumini wa siasa za upinzani na rasmi
alijiunga na Chadema.
Alisema ameamua
kujiunga na Chama hicho kutokana na ukweli kwamba ndicho chama kinachoonekana
kuwa chama chenye utu, misingi bora ya usawa, uheshimu wa haki za wanachama na
Watanzania pamoja na mshikamano.
“Kwa furaha kubwa
kabisa na penda kuchukua fursa hii kuwatangazia Wanambeya na umma wa Watanzania
kwa kuvunja ukimya na sasa natangaza kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi na
nisema kuwa huu ni mwanzo tu mimi nimetangulia na wengine watakuja au kufuata
hatua kwa hatua”alisema Mwamalala.
Hata hivyo, Mwamalala
alipinga kuwa alifukuzwa chama bali kilichotokea ni kwamba mwanzoni mwa Januari
3 mwaka huu alitangaza kujiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya Chadema ikiwa
ni pamoja na kujivua uanachama wa chama hicho.
Pamoja na kudai kuwa
hajafukuzwa, taarifa za Chama hicho zinaeleza kuwa Mwamalala alifukuzwa
uwanachama tangu mwaka jana.
No comments:
Post a Comment