Andy Murra akinyanyua juu taji lake la ubingwa wa Brisbane International 2013
BRISBANE, Australia
NYOTA wa tenisi raia wa
Uingereza, Andy Murray jana Jumapili amefanikiwa kuutetea ubingwa wake wa Brisbane
International kwa ushindi wa seti mfululizo, dhidi ya mpinzani wake Grigor
Dimitrov.
Murray, bingwa wa Michuano ya
Wazi ya Marekani ‘US Open’ na kinara wa mchezo kwa viwango vya ubora, aliibuka
mbabe kwa 7-6 (7-0) 6-4 katika mechi iliyopigwa kwa saa moja na nusu, dhidi ya
Dimitrov raia wa Ubelgiji anayeshika nafasi ya 48 ya ubora.
Haikuwa rahisi kwa Mskochi
Murray kuibuka na ubingwa huo, akifanya kazi ya ziada kutoka nyuma kumuwezsha
kuongoza hadi nusu ya kwanza na kuja kushinda.
Murray alitinga kirahisi
fainali ya michuano hiyo baada ya mpinzani wake katika mechi ya nusu fainali,
Kei Nishikori kujitoa mchezoni kutokana na kuumia goti.
Murray aleyecheza fainali akiwa
anashikilia nafasi ya tatu kidunia kwa ubora wa tenisi na namba moja kwa
Uingereza, alirudi vema kutoka mapumziko na kutoka nyuma na kushinda 6-4 katika
mechi za seti tano mfululizo.
Murray alikuwa katika michuano
ya Brisbane International, kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mashindano
ya Wazi ya Australia ‘Australian Open’, yatakayofanyika kwa wiki mbili kuanzia
Januri 14 hadi 27, jijini Melbourne.
No comments:
Post a Comment