Demba Ba
Fernando Torres
LONDON, England
"Wanaweza kucheza
pamoja safu ya mbele ya Chelsea. Ba alikuwa akicheza akiwa na Papiss Cisse
katika kikosi cha Newcastle, hivyo yeye anaweza kabisa kucheza ushambuliaji
pacha"
KOCHA Rafael Benitez amesema
haoni sababu kwa nini washambuliaji wake Demba Ba na Fernando Torres wasiwezer
kucheza pamoja kwa mafanikio, kauli aliyopitoa baada ya Ba kufunga mara mbili
katiika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge Chelsea.
Ba, juzi lifunga mara mbili
katika pambano la raundi ya tatu ya Kombe la FA, kuiwezesha Chelsea kuiondosha
mashindanoni Southampton, kwa mabao 5-1 mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa St
Mary’s.
Huku Torres akianzia benchi
katika mechi hiyo ya Jumamosi, Ba ilimchukua takribani dakika 35 kufunga bao
lake la kwanza kabisa akiwa na Chelsea, ambalo lilikuwa la kusawazisha na
kufungua mvua ya mabao baadaye.
"Wanaweza kucheza pamoja
safu ya mbele ya Chelsea," alisema Benitez baada ya mechi hiyo.
"Ba alikuwa akicheza
akiwa na Papiss Cisse katika kikosi cha Newcastle, hivyo yeye anaweza kabisa kucheza
ushambuliaji pacha na mwenzake kwa sababu ni mchezaji mjanja, lakinipia
inategea na mfumo wa mchezo na nyota anaoshirikiana nao.
"Napendelea tatizo hili
la kuwa na washambuliaji wawili, kuliko kupaswa kuwa na mmoja anayetakiwa kuwa
makini mchezoni kwa dakika zote.
"Jambo muhimu kwa timu ni
kuwa na wigo mpana wa uteuzi wa kikosi. Wao ni wachezaji wazuru na kimsingi
wanaweza kupambana, au labda tunaweza kuwaongoza wao pamoja – inategemea na
mchezo."
Ba alifunga bao moja katika
kila kipindi, katika mechi ambayo kulikuwa na mabao kutoka kwa Victor Moses,
Branislav Ivanovic na penati ya dakika za lala salama ya Frank Lampard.
"Ni muhimu mno kwa
mshmabuliaji kufunga mabao, mengi zaidi awezavyo, lakini zaidi ni kwana nmna
gani ushirikiano wake na timu unakuwa na uelewa alionao katika kuweza kutambua
nini tunatarajia ambavyo vyote vimeniridhisha," alisema Benitez.
"Alionesha uzuri wake
mbele ya lango na kila alichofanya dimbani katika mechi hii kilinivutia na
kuniridhisha vya kutosha. Alikuwa mjanja mno mchezoni."
Aidha, bao la mtokea benchi Lampard
katika mechi hiyo, lilimfanya aifikie rekodi ya utikisaji nyavu mara nyingi
zaidi katika klabu hiyo kwa kufikisha mabao 193 na kumpiku mshikilia rekodi
hiyo wa kudumu Kerry Dixon anayeshika nafasi ya pili sasa.
No comments:
Post a Comment