Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa RnB Tanzania, Benard Paul
‘Ben Pol’ amesema amelazimika kuchelewa kutoa video ya wimbo wake wa
‘Yatakwisha’ aliomshirikisha Estelina Sanga ‘Linnah’ kutokana na mabadiliko ya
mfumo wa Analogia na kwenda Digitali.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es
Salaam, Ben Pol alisema amelazimika kufanya hivyo kutokana na mabadiliko hayo
ambayo kwa kiasi kikubwa yanawaumiza Watanzania wengi kutokana na gharama za
kugharamia Digitali ili uweze kuangalia vipindi mbalimbali katika televisheni
yako.
Ben Pol alisema, video ya wimbo huo anatarajia
kuiachia mwanzoni mwa mwezi Aprili ambapo anaamiki kwa kisi kikubwa Watanzania
watakua wameizoea hali hiyo.
“Unajua Ving’amuzi vinapatikana kwa bei ya juu
sana sio kila mtu ambaye anauwezo wa kukipata, kwasasa nikiachia video hii
najua haitapokelewa vizuri na mashabiki wangu kwasababu asilimia kubwa watakua
wanasimuliwa kuliko wanaoangalia,” alisema.
Pia alisema, kutokana na kazi yake ya ‘Pete’
kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio, anaona haina ulazima wa
kuifanyia video kazi hiyo ila amewapa vionjo kidogo ndani ya video ya
‘Yatakwisha’.
“Unajua audio ikifanya vizuri inakua inatosha
hamna ulazima wa kuangaika na video kwaupande wangu naona kama itakuja kuharibu
kwasababu yenyewe inaweza isipokelewe vizuri, ila nimeweka baadhi ya vionjo
katika wimbo wa ‘Yatakwisha’ nnhivyo mashabiki wangu hawataikosa kabisa,”
alisema Ben Pol.
No comments:
Post a Comment