Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid
Ramadhan ‘Tunda Man’ amesema amekamilisha kalenda yake ya mwaka 2013 ambayo
itamuwezesha kufanya kazi zake katika mpangilio mzuri.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Tunda alisema
kila anapoingia mwaka mpya huwa anatabia ya kupanga ratiba ya mwaka mzima kwa
lengo la kufanya kazi zake katika mpangilio mzuri.
“Unajua hii inasaidia kufanya kazi zako vizuri
kutokana na kujua siku gani unafanya nini, kwahiyo unajipanga kwaajili ya siku
hiyo mimi naamini nikiwa najua siku Fulani naenda kufanya shoo sehemu lazima
nitajiandaa na kufanya mazoezi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuchagua nyimbo
ambazo najua nikiziimba nitawafurahisha mashabiki wangu na sio kukurupuka tu,” alisema Tunda Man.
Alisema anawaomba mashabiki wake wakae mkao wa
kula kupokea vitu vizuri kutoka kwake, na kwamba anajipanga kuachia kazi yake
mpya ambayo hajataka kuitaja jina kutokana wizi uliopo hadharani kati ya
wasanii wenyewe pamoja na waharamia katika tasnia ya muziki huo.
Tunda Man anatamba na kibao chake cha ‘Demu sio’
mbali na kuwa na kazi nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika
vituo mbalimbali vya redio na runinga.
No comments:
Post a Comment