Picha tofauti zinazoonesha tukio la Eden Hazard kumpiga muokota mipira
'Ball-boy' wakati wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Capital One, kati
ya Chelsea na Swansea City iliyoisha kwa sare ya 0-0. Hazard alilimwa
kadi nyekundu kwa tukio hilo, ambalo sasa ameomba radhi rasmi.
LONDON,
England
“Kijana aliukumbatia
mpira nami nilikuwa najaribu kuupiga mpira. Na nadhani niliupiga mpira kama
nilivyokusudia na sio kijana yule kama
ilivyotafsiriwa. Hata hivyo naomba radhi kwa hilo”
NYOTA wa Chelsea, Eden Hazard, amelazimika kukiri kosa na
kuomba msamaha, baada ya ‘kujisababishia’ kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa
kumpiga teke muokota mipira ‘ball-boy’ wakati wa mechi ya Kombe la Capital One dhidi
ya Swansea City juzi usiku.
Hazard raia wa Ubelgiji, alionekana akimpiga shuti la mbavu Charlie
Morgan, 17, ambaye ni mtoto wa Mkurugenzi wa Swansea Martin Morgan, ambapo
baadaye jana alisema hakumpiga kijana huyo.
"Kijana aliukumbatia mpira nami nilikuwa najaribu
kuupiga mpira. Na nadhani niliupiga mpira kama nilivyokusudia na sio kijana
yule kama ilivyotafsiriwa. Hata hivyo naomba
radhi kwa hilo.
"Kijana huyo alikuja katika vyumba vya kuvalia nguo
(baada ya mchezo) na tulizungumza mengi ikiwamo kumuomba naye kuniomba radhi na
kimsingi tulisameheana vizuri. Limeisha. Naomba radhi," alisema Hazard.
Tukio hilo
lilitokea dakika ya 78 ya mchezo huo ulioisha kwa sare ya 0-0, ambapo
alionekana kuufuata mpira kwa taratibu, kitu ambacho kilimsukuma Hazard
kukimbilia mpira ili kuwahisha mchezo, na kujikuta akigombea mpira huo na
kijana huyo.
Mwamuzi wa pambano hilo,
Chris Foy alimuonesha mkali huyo kadi nyekundu, na kumtoa mchezoni, kadi
inayoweza kumuweka nje ya dimba kwa mechi tatu zilizo chini ya Chama cha Soka
(FA).
…..The Sun/BBC……
Vеrу nice artіcle, ϳust what I was lοoking fοг.
ReplyDeleteAlso see my site :: chalkboards