LONDON,
England
Orodha ya klabu 10 tajiri zaidi na pato lao kwenye mabano
ni: Madrid (512.6), Barcelona
(483), Man Utd (395.9), Bayern Munich (368.4), Chelsea
(322.6), Arsenal (290.3), Man City (285.6), AC Milan (256.9), Liverpool
(233.2) na Juventus (195.4)
MABINGWA wa La Liga Real Madrid, wamebaki kileleni miongoni
mwa klabu tajiri duniani inakoongza ‘Ligi ya Fedha’ baada ya kuwa klabu ya kwanza
katika soka kukusanya zaidi ya Euro milioni 500 kwa msimu.
Mapato ya euro milioni 512.6 (sawa na pauni milioni 430.4) kwa
msimu uliopita wa 2011/12, umewafanya Madrid
kuongoza orodha ya klabu tajiri inayotolewa Deloitt kwa msimu wa nane mfululizo
sasa.
Madrid imebaki kinara wa
orodha hiyo kwa mwaka wa nane sasa, huku mahasimu wao Barcelona wakishika nafasi ya pili na Manchester
United, wakikamata nafasi ya tatu, wakiwa ni vinara miongoni mwa klabu saba za
Ligi Kuu zilizoingia 20 Bora.
Pato la jumla la timu zilizoingia katika 20 bora ya klabu
tajiri duniani, limeongezeka kwa 10% na kufikia kiasi cha Euro bilioni 4.8.
"Hii inaonesha ni kwa namna gani watu wanaupenda mchezo
wao, na kuchangia ukuaji wa uchumi wake," alisema Dan Jones, kiongozi
kundi la kibiashara la Kampuni ya Deloitte, alipohojiwa na BBC Sport.
"Mchezo huu pendwa umeathiriwa na mtikisiko wa uchumi
unaoiandama michezo, hasa katika suala zima la haki ya utangazaji. Kuona ukuaji
wa pato la klabu 20 bora kwa asilimia 10 ni makuzi mema ya uchumi katika soka,
kwa miaka karibia 15 iliyopita."
Hata hivyo, Jones anatarajia kwamba, klabu zote Barcelona – ambayo pato lake limekua
kwa 7% hadi kufikia euro milioni 483 (sawa na pauni milioni 405.5) na Manchester
United zitavuka pato la jumla la euro milioni 500 katika miaka michache ijayo.
Orodha ya timu 10 bora na pato lao kwenye mabano ni kama
ifuatavyo: Madrid (512.6), Barcelona (483), Man Utd (395.9), Bayern Munich (368.4),
Chelsea (322.6), Arsenal (290.3), Man City (285.6), AC Milan (256.9), Liverpool
(233.2) na Juventus (195.4).
…..BBC…..
No comments:
Post a Comment