Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo
akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la kampeni maalum ya
kuadhimisha sikukuu ya wapendanao ‘ Valentine Day’ iliyoandaliwa kwa
kushirikiana na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha
televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM. Kushoto ni AFISA Masoko na Mauzo
wa AMG, Prosper Vedasto
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Push Media Mobile
inatarajiwa kutoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya sh milioni 8 kwa
mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao ‘Valentine Day’
inayoadhimishwa Februari 14 kila mwaka.
Hayo yalisemwa jijini Dar es
Salaam Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo,
katika uzinduzi wa kampeni hiyo pamoja na Kampuni ya African Media Group (AMG),
kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.
Rugambo alisema kuwa, wameamua
kutoa zawadi hiyo kubwa ili kuwafanya wapendanao wengi kushiriki na kupata
nafasi ya kushinda.
Alisema kuwa, ili kuingia
katika droo ya shindano hilo, unatakiwa kutuma neno ‘Penzi’ kwenda namba 15678
na kujibu maswali mbalimbali yahusiyo masuala ya mapenzi na siku ya Valentine.
“Hii ni promosheni ya kwanza
kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu
kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile vile kuwazawadia wadau wetu kwa
kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa, mbali ya zawadi
hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kujishindia kompyuta
(Laptop), aina ya HP yenye thamani ya sh milioni 1.5, simu aina ya Blackberry
Curve yenye thamani ya sh 500,000 na ‘Home Theatre’ ya thamani ya sh 400,000.
Kwa mujibu wa Rugambo, lengo
lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao kuwa kubwa kama nyingine, kwani
mapenzi ni kitu muhimu katika maisha ya kila siku.
Alisema kuwa, mipango yao ni
kuwekeza katika sikukuu hiyo, ambayo jamii imeanza kuitilia mkazo japo si siku
ya mapumziko kama sikukuu nyingine, ambako mwaka huu, wameweka bajeti ya sh
milioni 30 ili kufanikisha zaoezi hilo.
No comments:
Post a Comment