HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2013

WANANCHI Wataka Maghembe akaone Madudu ya Mradi wa Maji wa Bil. 2/- unavyochezewa



Na Bryceson Mathias, Mvomero

WANANCHI wa mji mdogo wa Mvomero wamemtaka Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe (pichani) aende katika mji huo akajionee madudu ya mradi wa maji wa zaidi ya Bilioni mbili unavyochezewa, huku wao wanapata shida ya maji.

Kauli hiyo ilitolewa Januari 15, 2013 na wakazi wa Mji huo waliokuwa mto Mvomero na mwandishi kuwahoji kwa nini wanaoga, kufua na kuchota maji hayo hayo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ambapo walidai madudu na kero ya Mradi wao wa maji umewafikisha hapo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanaume na wanaume waliokuwa wakitoka kuoga, kufua na kuchota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani walisema, kwa hali ya shida ya maji safi ambayo wakazi wa mvoero tumefikia, tunamtaka Waziri wa Maji Prof. Maghembe aje ajionee madudu ya mradi wao wa maji wa Bilioni mbili unavyochezewa, ilihali wao wanapata shida.

“Mradi huu ulianza Januari 2012 na ulitakiwa ukabidhiwe mwaka jana June 6, 2012, lakini sasa umesimama na haujulikanai utaishi lini ndiyo maana tunalazimika kuoga, kufua na kuchota maji ya kunywa hapa hapa. Je mwandishi unadhani twenda wapi?”.

Mwanamke mmoja Mama Lishe kwa niaba ya wenzake alisema, Baba; Mimi ni Mama Nitiliye kama unavyoniona, kama naona Mitambo imelala haifanyi kazi, unanitaka niamini na kujidanganya kuwa maji yatakuja wakati hayapo? Ukitaka maji ya visima vya watu, lazima ununue!.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Mvomero waliozungumza na mwandishi kama nao wanapata shida ya maji walikiri na kusema, mara kadhaa wakiwauliza viongozi wa Kata wanawaambia kuwa, Mkandarasi amesimama kufanya kazi kutokana na kutolipwa kwa wakati, na pia wanadai aliongezewa Mkata hadi Januari mwaaka huu lakini hatuoni, hapa kuna ujanja.

Aidha Mwandishi alimtafuta Diwani wa Kata ya Mji Mdogo wa Mvomero Selemani Mwinyi (CCM) alikiri Mradi kusimama na kuwepo kwa Kampuni ya Kichina ya CCECC ambayo imeshafanya kazi Asilimia 88% na kulipwa takribani Milioni 600/-, na pia alieleza ipo Kampuni ya Ushauri ya Kimisri ya AAA-Consulting Engineer yenye Mhandisi.

“Hata mimi nashangaa Mradi kwa nini hauishi licha ya kuongezewa muda. Malipo kwa wakandarasi yanachelewa, vyombo vimesimama, kazi haifanyiki, hivyo hata mimi sijui kama fedha hiyo ipo au kuna mchezo mchafu sielewi!! Naungana na wananchi Waziri aje awapatie majibu”. alisema Diwani Mwinyi baada ya kubanwa.

No comments:

Post a Comment

Pages