Picha toka katika mtandao wa Youtube ikimuonesha Mohammed Hourani
enzi za uhai wake
AFP/YouTube/Al-Jazeera
DAMASCUS, Syria
Mwandishi wa habari wa kituo cha
Televisheni cha Al Jaazera Mohammed Hourani ameuawa jana ijumaa baada ya
kupigwa risasi alipokuwa akiripoti kuhusu mapigano yanayoendelea kuitikisa nchi
ya Syria.
Al Jaazera yenye makao makuu nchini
Qatar imethibitisha taarifa za kifo hicho na kusema kuwa Hourani alikutwa na
umauti baada ya kupigwa risasi na vikosi vinavyomtii Rais wa Syria Bashar al
Assad.
Hourani ameuawa siku
moja baada ya Mwandishi wa habari mwingine raia wa Ufaransa Yves Debay kuuawa
kwa kupigwa risasi kaskazini mwa nchi hiyo katika mji wa Aleppo.
Kwa mujibu wa Shirika
la Habari la Ufaransa AFP na Shirika la Waandishi wa Habari wasiokuwa na mipaka
lenye makao yake makuu jijini Paris Ufaransa, Waandishi wa habari wapatao 20
wameripotiwa kuuawa tangu kuzuka kwa mapigano ya kuung'oa madarakani utawala wa
Rais Bashar al Assad mwezi machi mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment