MUNICH,
Ujerumani
"Kama kipaumbele chake kingekuwa ni pesa, basi ni
wazi Bayern isingekuwa na nafasi ya kupata saibni yake. Nadhani yeuye alivutiwa
na sera, mtazamo na dira yetu kwa ujumla"
MWENYEKITI wa Klabu ya Bayern Munich ya hapa, Karl-Heinz
Rummenigge, amesemea kuwa, pesa haikuwa kipaumbele cha Pep Guardiola kukubali
kuingia mkataba wa kuinoa Bayern Munich kuanzia majira ya joto.
Guardiola, 41, aliyekuwa kocha wa zamani wa FC Barcelona, juzi
alitangazwa kuwa kocha mpya wa Bayern na kuingia mkataba wa miaka mitatu ya
kufanya kazi na klabu hiyo ya Allianza Arena.
Lakini wakati Guardiola akiukubali kuingia mkataba huo na
Bayern, alikana ofa nono zenye vitita vikubwa kutokla klabu za England zikiongozwa na Chelsea
na Manchester City.
"Kama kipaumbele chake
kingekuwa ni pesa, basi ni wazi Bayern isingekuwa na nafasi ya kupata saibni
yake," alisema Rummenigge.
"Nadhani yeuye alivutiwa na sera, mtazamo na dira yetu
kwa ujumla. Bila shaka huilo litamuwezesha yeye kupata euro chache sana akiwa hapa, lakini kama
pesa ingekuwa ndio kila kitu kwake, asingekubali kusaini kuja hapa kuanzia
Julai 1."
Guardiola, ambaye atachukua mikoba ya kocha anayemaliza muda
wake Jupp Heynckes, alikuwa ni kocha aliyevutia klabu nyingi tangu alipoamua
kuachia ngazi kuinoa Barcelona
kiangazi kilichopita, aliyotwaa nayo jumla ya mataji 14 katika misimu minne.
Aliamua kukaa pembeni katika jukumu la kuinoa klabu yoyote
kwa msimu mmoja, lakini hiyo haikuzifanya klabu klutosaka saini yake kwa udi na
uvumba, vita ambayo Bayern imeibuka mshindi hatimaye.
Chelsea, Manchester United, Manchester City, AC Milan, Roma
na Paris St Germain, kwa nyakati tofauti ziliripotiwa na kukubali kuwa zinasaka
saini ya Guardiola, kiungo wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania.
……The Sun……
No comments:
Post a Comment