LONDON,
England
Wenger alikuwa katika
wasiwasi mkubwa wa kumpoteza mkali huyo, kama ilivyokuwa kwa kina Cesc
Fabregas, Samir Nasri, Robin van Persie na Alex Song waliotimka zao katika
kipindi cha majira ya joto ya miaka miwili iliyopita
WINGA hatari wa kimataifa wa England, Theo Walcott hatimaye
amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Arsenal.
Walcott, 23, alikamilisha usajili huo jana kwa kurefuisha
mkataba wake kwa miaka mitatu na nusu utakaomuwezesha kupokea mshahara wa pauni
100,000 kwa wiki akiwa na klabu hiyo ya Emirates.
Jioni ya juzi Alihamisi bosi wake Arsene Wenger
alithibitisha: “Nina matumaini makubwa ya kumsainisha mkataba huo kabla ya
mwisho wa wiki. Kuna uwezekano mkubwa wa kufanyika hilo. Matumaini niliyonayo juu ya ukamilifu
wa hilo ni
asilimia 99 sasa.”
Wenger alikuwa katika wasiwasi mkubwa wa kumpoteza mkali
huyo wa safu ya mbele kama ilivyomtokea kwa
nyota kadhaa klabuni Emirates, baada ya mktaba wake kuelekea ukingoni huku
akigoma kusaini mpya akishinikiza ongezeko la mshahara wake.
Tayari huko nyuma bosi huyo wa Gunners alishashuhudia wakali
wake kama Cesc Fabregas, Samir Nasri, Robin
van Persie na Alex Song wakitimka zao katika kipindi cha majira ya joto ya
miaka miwili iliyopita.
Na Wenger hakuficha ukweli juu ya hilo, ambapo alikiri:
“Ndio nilikuwa na wasiwasi sana wa kumpoteza, kwamba angeweza kuondoka Emirates
kwa sababu nina uzoefu wa kutosha wa aina ya mazungumzo na makubaliano
tuliyokuwa tukifanya na yeye.
“Wakati jambo moja linapodumu kwa muda mrefu kwenye
majadiliano, kamwe hilo
halina ishara nzuri kimatokeo.
“Na ilituichukua muda mrefu kutufikisha pale sisi tulipotaka
kufika kimazungumzo kutuwezesha kupata tulichohitaji. Hili halijamaliziika
rasmi, lakini nina matumaini makubwa ya kulimaliza hilo wikiendi hii.”
Kukamilika kwa usajili wa Walcott aliyekuwa akiwindwa na
klabu kadhaa za England
na nje ya nchi hiyo, kunampa fursa Wenger ya kugeukia soko la usajili wa majira
ya baridi baranmi Ulaya, lililofunguliwa Januari 1.
……….The Sun/Daily Mail………..
No comments:
Post a Comment