MADRID, Hispania
“Ni uongo kabisa kwamba mimi, nahodha na Mkurugenzi Mkuu
tulikutana wakati wa chakula cha mchana, kwa ajili ya pamoja na mambo mengine
kumjadili Mourinho kama kocha”
REAL Madrid juzi usiku imelazimika kukanusha habari
zilizoripotiwa na vyombo vya habari kuwa iliwauliza wachezaji wake nyota na
waandamizi kama imfukuze kazi majira ya joto kocha wao Jose Mourinho.
Rais wa Madrid, Florentino Perez (pichani kushoto) ameyakana madai kwamba
nahodha wa Galacticos, Iker Casillas na Sergio Ramos wamemwambia kwamba
wachezaji nyota kikosini wataomba kutimka Bernabeu, kama klabu itaendelea kuwa
chini ya Mourinho msimu ujao.
Perez alisema: “Ni uongo kabisa kwamba mimi, nahodha na
Mkurugenzi Mkuu tulikutana wakati wa chakula cha mchana, kwa ajili ya pamoja na
mambo mengine kumjadili Mourinho kama kocha.
“Uliochapishwa magazetini ni uongo wenye nia ya kutibua
utulivu wa klabu yetu,” aliisistiza Perez.
Mourinho ameripotiwa kugombana na wachezaji nyota wa Madrid,
wakiwamo Cristiano Ronaldo, Ramos, Pepe, Mesut Ozil, Fabio Coentrao na
Casillas, ambaye atakosa mechi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man United baada ya
kuumia mkono wa kushoto.
Kutokana na kuumia na kutarajiwa kukosekana kikosini kwa Casillas
langoni, Mourinho amedaiwa kufikiria kutoa dau nono la pauni milioni 10 kuwania
saini ya mlinda mlango wa Spurs, Mfaransa Hugo Lloris ama Mbrazil wa QPR, Julio
Cesar.
….The Sun…..
No comments:
Post a Comment