“Haikuwa rafu kabisa,
kwa sababu hatuwezi kupoteza mchezaji wetu muhimu kwa mechi tatu mfululizo bure
hivi hivi bila sababu. Ni wazi kwamba haikustahili kuwa kadi nyekundu,
tunajiandaa kuikatia rufaa”
MAKOCHA wa klabu Manchester
City , Roberto Mancini na
wa Arsenal, Arsene Wenger, wameonesha hasira zao kwa kadi nyekundu za moja kwa
moja waalizooneshwa mabeki wao Vincent Kompany na Laurent Koscielny wakati klabu zao
zilipoumana juzi.
Mancini bosi wa mabingwa wa soka England , ameipinga vikali kadi ya
mwamuzi Mike Dean kwa nahodha wake Kompany, anayodaiwa kupta kutokanana rafu
kwa kiungo wa Gunners, Jack Wilshere, huku akisema klabu inajiandaa kuikatia
rufaa.
“Haikuwa rafu kabisa, kwa sababu hatuwezi kupoteza mchezaji
wetu muhimu kwa mechi tatu mfululizo bure hivi hivi bila sababu. Ni wazi kwamba
haikustahili kuwa kadi nyekundu.
“Kompany aliingia akiwania mpira, ingetegemea kama mpinzani angewahi kuuchukua mpira kabla. Sijui
inawezekanaje kwa mchezaji kuambulia kadi nyekundu ya moja kwa moja kama hii aliyopewa nahodha wangu,” alisisitiza Mancini.
Kompany alioneshwa kadi nyekundu hiyo na mwamuzi Dean,
katika dakika ya 75 ya pambano hilo
la Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Emirates, lililoisha kwa Gunners kulala nyumbani
kwa mabao 2-0.
Mapema katika pambano hilo ,
beki Mfaransa wa Arsenal, Koscielny alitolewa nje ya dimba kwa kadi nyekundu,
baada ya kufanya madhambi kwa kumzuia isivyo halali mshambuliaji Edin Dzeko asifunge
bao.
Wenger aligeuka mbogo na kuilalamikia kadi hiyo, akisema:
“Ilinishangaza sana
kusema ukweli. Kwa hakika. Nilikataa kuangalia tena marudio ya tukio lile kwa
sababu ni kwa kiasi gani limetusaidia hivi sasa?
“Tunaishia kwa kufuata maamuzi ya marefa na kufanya mengi
zaidi ya hayo. Nasikia ilikuwa ni penati hatimaye kwa maamuzi ya refa. Ilikuwa
kadi nyekundu, Sijui chochote juu ya hilo .”
Kutokana na kadi nyekundu ya Kompany, inamaanisha nahodha
huyo atalazimika kukaa jukwaani wakati wa mechi mbili za Man
City za Ligi Kuu dhidi ya Fulham na
QPR, pamoja na mechi ya raundi ya nne ya Kombe la FA, dhidi ya Crystal Palace au Stoke.
No comments:
Post a Comment