Waendesha Boda Boda wakilalamikia na kujadili vitendo vya kodi na kukamatwa ovyo.
Na. Bryceson Mathias, Mvomero
Madereva na Wamiliki wa
Pikipiki maarufu kwa Jina la Bodaboda, wameilalamikia Mamlaka ya Mapato (TRA)
Mji Mdogo wa Madizini na Kampuni ya Udalali ya MEM Auction Mart, wakiituhumu
kuwanyanyasa na na wakati mwingine kuwadai Rushwa wanapofanya kazi yao ya kuwakagua
na kukamata vyombo vyao.
Malalamiko hayo yalitolewa na Wadau jana
kufuatia kuwepo kwa kamata Kamata ya Ukaguzi dhidi ya Uhalali wa Vyombo hivyo,
iwepo vmetimiza masharti yote yanatpaswa kutimizwa ili viweze
kutumika kuwahudumia wananchi bila kuwa na kasoro zinazoweza
kusababisha matatizo miongoni mwa Jamii.
Baadhi ya Wenye Vyombo na Madereva waliokaguliwa
walidai kwamba, pamoja na kuwa na Vielelezo vinavyostahili kuwa navyo, kuna
akati walilazimishwa kuwasilisha vyote kwa wakati huo na kutakiwa kuacha vyombo
vyao hapo, na kutishiwa kama vikilala watalazimika kulipia Shilingi 20,000/-
kila Chombo jambo walilodai ni kuwanyanyasa.
“Tulikamatwa na kutakiwa kuwasilisha nyaraka
zote hata zile ambazo zinatakiwa kutunzwa nyumbani, wamedai walisumbuliwa kiasi
kubaini kwamba wanafanyiwa hivyo ili yu mkini kuwalazimisha atoe chochote ili
waondoke na wengine kudai walilfikia kudaiwa Shilingi 10,000/- Ili
waachiwe”.alisema mmoja wao aliyeombwa asitajwe jina.
Ofisa wa TRA Mji Mdogo wa Madizini, Salum
Mwanamsha alipoulizwa kuhusu Malalamiko hayo alisema, Kazi ya Ukaguzi wa vyombo
hivyo haifanywi na TRA bali kuma Kampuni ya Udalali ya Mem ambapo dai la kuwepo
kwa harufu ya rushwa hawezi kuisemea.
Mmoja wa watendaji mwenye Namba ya Simu
0715-413736 alimwandikia mwandishi ujumbe mfupi kati ya jumbe mbili za vitisho
ukisema,
“Naomba umlete huyo au ww kuhusu tuhuma ya kutoa
elfu 10 ili pikipiki itoke, maana hiyo piikipiki ameitoa Salum wakati mm sina
ruhusa ya kutoa name nimesikitishwa na tuhuma mnanizushia na swla hili
nitalifikisha mbele ya sheria naijua pikipiki ninamtafuta aje athibitishe kauli
mnazonizitoa”
Awali Wananchi wenye vyombo wakiwemo Madereva wa
Bodaboda walilalamika kwamba, ‘Pamoja na Dereva wao ambaye ni Mkuu wa Msafara
katika kukamata Pikipiki, walikuwa wanaingia hadi ndani Chumbani wakiwa na
Polisi mwenye Bundukisema, jambo ambalo lilionekana kuwaudhi watendewa na
kulitolea malalamiko’.
No comments:
Post a Comment