Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa bongo
fleva nchini, Ally Mohamed ‘Z Anto’ amesema kwa mwaka huu amejipanga kurudi
upya katika tasnia hiyo kutokana na kuwa na ngoma kali katika maktaba yake.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Z. Anto alisema ana azina kubwa ya nyimbo huku akiwa anatafakari
ni nyimbo ipi aanze kuiachia kutokana na kila moja kuwa katika kiwango cha juu.
“Kwa sasa natakari namna
nitakavyoachia nyimbo zangu kutokana na kila moja kuwa katika kiwango cha juu,
hivyo najaribu kukaa na watu wangu wa karibu ili wanishauri ni nyimbo ipi ianze
kwenda hewani na kufuata nyingine,” alisema Z.Anto.
Nyota huyo aliyezaliwa 1998
jijini Dar es Salaam aliwahi kutamba na nyimbo mbalimbali kama Kisiwa cha
Malavidavi, Mpenzi Jini, Imani Sina, Mpenzi Spesho, Chakula Changu zilizompa
umaarufu pamoja na mafanikio makubwa.
Z. Anto anawaomba mashabiki
wake kukaa katika mkao wa kula wakisubiri kazi mpya ambazo zipo katika ubora wa
hali ya juu kwa lengo la kuhakikisha anaridisha adhi ya awali ambapo alikuwa
gumzo Afrika Mashariki.
“Mashabiki wangu wakae mkao
wa kula kusubiri kazi zangu mpya ambazo ziko kwenye maktaba na wakati wowote
baada ya kutafakari nitaamua nianze kuachia wimbo upi ili afanikishe kukonga
nyoyo za wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini,” alisema.
No comments:
Post a Comment