Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi
kipya nchini Ambwene Yessaya ‘AY’ ameomba wadau mbalimbali pamoja na Serikali
kuhakikisha walimu wanapata huduma bora katika vitendea kazi na kuboreshewa
mishahara yao.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam na Habari Mseto Blog, AY alisema walimu wengi wapo katika mazingira magumu ya
ufundishaji kutokana na baadhi yao kutokuwa na vifaa vya kufundishia hali
ambayo inafanya kutotoa elimu bora kwa wanafunzi ambao nguzo kwa taifa.
“Nimepita katika shule nyingi
na nimegundua kuwa wanachangamoto za vifaa vya kufundishia pamoja na ukosefu wa
mishahara bora kitu ambacho kinatakiwa kufanyiwa kazi mapema ili kuhakikisha
wanafunzi wanapata huduma bora na inayostaili,” alisema AY.
Pia nyota huyo alisema kuwa
katika kipindi yuko katika harakati za kuachia kazi tofauti ili kuwaonesha
wapenzi na mashabiki kuwa yuko katika hatua nyingine ya kimataifa ambayo
inapaswa kuigwa na kila msanii ili kuhakikisha bendera ya Tanzania ina pepea
vizuri katika anga za kimataifa kupitia muziki.
“Mashabiki wangu wakae mkao
wa kula kutokana na kazi ambazo nimeziandaa kwa mwaka huu, baadhi yake ziko
katika hatua za mwisho kukamilisha na moja ya kazi hiyo ni wimbo ambao mpya
ninaoutarajia kuuachia Februari mwaka huu,” alisema AY.
No comments:
Post a Comment