HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 19, 2013

Aliyetelekezwa na Mume achoshwa kulea watoto, ataka kunywa sumu afe


 Monika Akipekua Nyarayi akajifungua mtoto wa tatu Yeremiea baada ya kutelekezwa akiwa na Miimba ya Miezi 5
Monika Isaya (25) Aliyetelekezwa na watoto watatu na Mumewe Mkuyu Juma aliyekuwa akifanya kazi Basi la Bin Salum, wakizurula mitaani

Na Bryceson Mathias, Morogoro

MKAZI wa Hembeti Mvomero Monica Isaya (25) aliyetelekezwa na Mumewe Mkuyu Juma akiwa na Mimba ya Miezi Mitano ya Mtoto wa Tatu amesema, amechoshwa kulea watoto wake watatu waliozaa na mumewe kutokana na kushindwa kujikimu hivyo ameamua anywe sumu ili afe apate kupumzika.

Isaya alisema hayo alipohojiwa na Mwandishi hivi karibuni akiwa analia wakati akipita mitaani kutafuta Riziki, huku akiwaongoza watoto wake wawili wanaotembea,  Tatu Mkuyu (8), Ayubu Mkuyu (4) na Yeremeia Mkuyu (Miezi Miwlii) aliyebebwa mgongoni.

Akielezea kisa cha kutelekezwa Isaya alisema, “Nilikwenda kwenye Msiba wa Bibi Mzaa Baba Hembeti  MVomero, niliporudi nyumbani nilikamata Mume wangu Ugoni akiwa na Mke mwingine nyumbani mwetu, ambapo kesho yake alitoroka na mwanamke huyo na kwenda naye Dar es salaam na kunitelekeza na watoto wawili huku akiniacha na Mimba ya Miezi mitano”.alisema Isaya

Alisema Mumwe anaitwa. Mkuyu Ayubu Mweyeji wa Singida Kijiji cha Mnene ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye Basi la Abiria la Bin Salim linalofanya safari zake kati ya Dodoma na Dar es Salaam, na pia alidai tangu aondoke 8.12.2012 hajui Nguo za Watoto, Malazi, Chakula ila yeye ndiye aayehangaika hivyo kwa hivi sasa amechoka, uamuzi alionao  anaona heri anywe sumu afe kuliko kupata mateso.

Aliongeza kwamba, Nyumba waliyokuwa wamepanga na mumeo baada ya kuwatelekeza walishndwa kulipa Kodi kwa mwenye nyumba, naye akachukua Jukumu la kuwafukuza na sasa amehifadhiwa na Mama mmoja ambaye ameamua kumsaidia Bure yeye na watoto.

Mwanamke huyo amekuwa akiwatunza watoto hao kwa kufanya vibarua vya kumwaga Nzege ili awavishe, awalisha na kuwapa mahali pa kulala malaika wa Mungu hao, jambo ambalo limemfanya afa yake kuwa nyong’enyevu kutokana na kazi ngumu zinazomzidi uwezo.

Aidha Isaya ambaye alisoma Shule Sekondari Chamwino Ikulu 2002-2004 na kuishia Kidato cha Tatu baada ya kuugua na kushindwa kurejea Shuleni, baadaye hali yake iliimarika wenzake wakiwa wameshamaliza masomo, hivyo kufanikiwa kuolewa na Mkuyu ambaye amemtelekeza, huku akimtaja Baba yake kuwa ni Husulu Isaya na Marehemu mama yake ni Mahawi Shilonyana.

Hata hivyo alipoulizwa kama ana mawasiliano na mumewe alisema hana ila alimuachia simu Na. 0766-430026 akidai atakuwa anampigia, lakini alipiga siku mmoja akmtaka aongee na mke mwenzie jambo alilopata hasira akafuta Namba yake. Pia alisema amekwenda Ustawi wa Jmii hadi Polisi ili wamsaidie kutunza watoto au kumkamata wanasema wameshindwa kumpata na ustawi wanadai hawana la kumsaidia.

No comments:

Post a Comment

Pages