Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally
Timbulo ‘Timbulo’ anajipanga kuachia albamu yake ya kwanza inayokwennda kwa
jina la ‘Domo langu’ ambayo itakua na jumla ya nyimbo kumi.
Timbulo alishawahi kutamba na vibao vyake kama
Domo langu ambacho kimebeba jina la albamu hiyo, Timbulo wa leo, Samson na
Delila na vinginevyo ambavyo vinanfanya vizuri katika soko la muziki wa kizazi
kipya.
Akizungumza Dar es Salaam, Timbulo alisema
yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa albamu hiyo ambayo anaamini itafanya
vizuri katika soko la muziki hilo kutokana na nyimbo zilizobeba albamu hiyo.
“Namshuku mungu asilimia kubwa ya kazi zangu
zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu hivyo ninaimani hata kazi hii
itapokelewa vizuri kwani nyimbo zilizomo humo ni moto wa kuotea mbali,” alisema
Timbulo.
Alisema kwasasa anajianndaa kukamilisha kazi
yake ambayo nayo itakuwepo ndani ya albamu hiyo, inayokwenda kwa jina la
‘Lastiki ya upendo’ ambayo amewashirikisha wasanii wa kundi la Malea kutoka
Cameroon.
Msanii huyo kwasasa anatamba na ngoma yake ya
‘Bado kijana’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na
runinga kutokana na ujumbe uliobeba.
No comments:
Post a Comment