HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 11, 2013

IRAN WASHEREHEKEA MIAKA 34 YA MAFANIKIO

DAR ES SALAAM, Tanzania
 WATANZANIA leo wameungana na Jamhuri ya  Kiislam ya Iran katika kusherehekea miaka 34 ya mafanikio tangu  mapinduzi yaliongozwa na Kiongozi wa Kidini, Ayatollah Khomen yakumuondoa madarakani Mfalme Shah Pahlavi mwaka 1979.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam leo na Balozi wa Iran nchini Mehdi Agha Jafari, katika sherehe hizo ambazo zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje, akiwemo Rais wa awamu ya pili, Ali Hassani Mwinyi.

Alisema Wairan wanajivunia mapinduzi hayo kwani yamekuwa chachu ya misingi ya haki katika jamii ambapo pia yameweza kuifanya nchi hiyo kupiga hatua kimaendeleo hadi kutambulika kimataifa.

Jafari alisema mafanikio yaliopatikana baada ya mapinduzi hayo ni katika sekta za viwanda, afya, Teknolojia na upande wa kilimo.

Aliongeza kuwa nchi hiyo hivi sasa imefanikiwa kuzalisha awataalam wake, ambao wamefanikiwa kurusha vyombo vya kisayansi kwenda anga za juu.

“Hivi sasa nchi yetu inaviwanda vya kutengeneza dawa mbalimbali ikiwemo za binadamu pia upande wa kilimo hatuko nyuma tunazalisha zana za kilimo haya ndio mafanikio ya mapinduzi”alisema Jafari.

Aidha, nchi hiyo iliingia katika mapambano dhidi ya utawala wa Mfalme Shahah kwa zaidi ya miaka 20 kutokana na dhuluma, kujilimbikizia mali katika familia yake, kuua tamaduni za Wairan huku akiruhusu tamaduni za nchi za magharibi ambazo ni kinyume na nchi  hiyo.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha, akizungumza kwa niaba ya Waziri Berdard Membe ambaye yuko Dodoma kwa majukumu muhimu, alisema Tanzania itaendeleza ushirikiano na nchi hiyo, kwani ushirikiano wa nchi hizo mbili una historia ndefu hususan  kwa upande wa Zanzibar.

Vilevile wanaishurukuru nchi hiyo kwa misaada kwenye maeneo mbalimbli nchini yakiwemo ya Afya, kilimo, kielimu na mengine.

No comments:

Post a Comment

Pages