Seyodou Keita wa Mali katikati akichuana na mabeki wa timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana.
Wachezaji wa timu ya Mali wakishangilia ushindi dhidi ya Afrika Kusini
DURBAN, Afrika Kusini
Mali imerejea rekodi
ya kuwaondoa wenyeji wa fainali za Afcon, baada ya mwaka jana kutoka nyuma kwa
mabao 2-0 na kusawazisha, kisha kuwaondoa wenyeji Gabon waliondaa kwa pamoja na
Guinnea Ikweta
WENYEJI wa fainali za 29 za Kombe la Mataifa Afrika, timu ya
taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, jana usiku imeyaaga rasmi mashindano
hayo, baada ya kushindwa kutumia vema changamoto ya mikwaju ya penati.
Bafana Bafana ilijikuta ikiambulia penati 1-3 dhidi ya Mali,
hatua iliyokuja baada ya dakika 120 za kufungana bao 1-1.
Afrika Kusini ilikuwa ya kwanza kupata bao lake kunako
dakika ya 31, likiwekwa nyavuni na Tokelo Rantie aliyetumia vema ushirikiano wa
May Mahlangu na Thuso Phala.
Mali ilikuja juu kipindi cha pili na kufanikiwa ‘kuchomoa’
bao hilo kupitia nyota wa zamani wa FC Barcelona ya Hispania, Seydou Keita kwa
kichwa katika dakika ya 58, akiunganisha krosi ya Mahamoud Samassa.
Shujaa wa hatua hiyo kwa upande wa Mali alikuwa ni mlinda
mlango Soumbeyla Diakite, aliyepangua penati mbili za Bafana Bafana huku moja
ikipigwa nje na kuyeyusha ndoto wenyeji.
Mashujaa waliotikisa nyavu katika mechi hiyo na kuipaisha
Mali hadi nusu fainali walikuwa ni Mahamane Traore, Adama Tamboura na Cheik
Diabate.
Siphiwe Tshabalala akifunga penati pekee ya Bafana Bafana,
huku zile za Mahlangu na Dean Furman zikipanguliwa na kipa Diakite na
Lehlohonolo Majoro akipaisha mkwaju wake.
Mali imerejea rekodi ya kuwaondoa wenyeji wa fainali za
Afcon, baada ya mwaka jana kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kusawazisha na
kuwaondoa wenyeji Gabon waliondaa kwa pamoja na Guinnea Ikweta.
Kabla ya mpambano huo, timu ya Taifa ya Gha ilikuwa timu ya
kwanza kufuzu nusu fainali baada ya kuwang’oa Cape Verde kwa mabao 2-0 katika
fainali kali na ya kusisimua kwenye dimba la Nelson Mandela Bay.
Shujaa wa Ghana katika robo fainali hiyo alikuwa ni mtokea
benchi WakasoMubarak, aliyefunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 52, kabla ya
kufunga la pili dakika za majeruhi akitumia udhaifu wa kipa Cape Verde kuapnda
kushambulia kona.
……SuperSport.com…..
No comments:
Post a Comment