MANCHESTER, England
ROBERTO Mancini (Pichani kulia) anayeinoa Manchester City, ameshangaza
mashabiki wa soka kwa kusema yu tayari kubeba bendera ya rangi nyekundu na
nyeupe kuwashangilia mahasimu Manchester United katika mechi yao dhidi ya Real
Madrid, wiki ijayo.
Mtaliano huyo aliyeipa ubingwa wa England Manchester City
ana matumaini kwamba vinara na mahasimu wao Man United watafanya vema katika
pambano la mtoano wa 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya kikosi cha Jose
Jose Mourinho.
Mancini anaamini nafasi ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu
itakuwa kubwa, kama kikosi hicho cha Alex Ferguson kitasonga mbele katika
michuano hiyo.
Lakini dua ya Mancini anaomba wakati akiwatambua vema miamba
hiyo ya soka la Hispania na Ulaya kwa ujumla, baada ya kuwa alicheza na kikosi
hicho mara mbili katika hatua ya makundi ya michuano hii msimu huu.
Na yeye licha ya kusema atawaunga mkono, lakini amekiri kuwa
United inahitaji msaada wote inaohitaji kuweza kupata matokeo mazuri dhidi ya
Madrid.
Alipoulizwa kama angependa kuona Man United ikiichapa Madrid,
Mancini alisema: “Ndiyo, itakuwa mechi mbili nyingine dhidi yao. Nitakwenda
huko na kuwaunga mkono nikiwa na bendera nyeupe na nyekundu ya United.
“Lakini kucheza na Madrid ni ngumu mno, wao ni moja ya timu
bora kabisa duniani kwa sasa. Wao pamoja na mahasimu wao Barca. Wana wachezaji
wazuri, lakini pia historia ya kuvutia. Itakuwa ngumu mno kwa United kuwafunga
Madrid, kwa sababu klabu yao iko juu.”
Akizungumzia pengo la pointi alilonalo dhidi ya vinara Man
United, Mancini alisemma: “Kama tuliweza kutwaa ubingwa msimu uliopita ambao
walikuwa kileleni kwa point inane mechi sita kabla ya kumaliza msimu, iweje
tushindwe mwaka huu kukiwa na mechi 14 kumaliza ligi?”
……The Sun/BBC……
No comments:
Post a Comment