Na Bryceson Mathias, Mvomero
KAYA 53 hazina makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa Mabati na zingine kubomoka katika Kijiji cha Makuyu wilayani Mvomero, kufuatia Mvua Kali iliyonyesha usiku kwa masaa Manne tangu saa Saba hadi saa 11.00 alfajiri, ambapo watu watatu walijeruhiwa na mmoja kuumwa na nyoka wakati akijiokoa.
Akizungumza na mwandishi leo Diwani wa Kata ya Mvomero Selemani Mwinyi amethibitisha kuezuliwa Mabati, kubomoka kwa nyumba na kujeruhuwa kwa watu hao na kwamba hakuna kifo kilichotokea isipokuwa wananchi wanahitaji chakula na Mahema.
Akielezea Madhara ya tukio hilo Mwinyi alisema, alisema Bw. Rashid Ally aliyeangukiwa na Matofali ya nyumba alishonwa nyuzi Nane kwenye Zahanati, Bw. Cheka Mawange aliumwa na Nyoka wakati akijaribu kukimbia ili kujiepusha asiangukiwe na nyumba na kutibiwa na dawa za kienyeji, na mmoja ambaye jina lake halijapatikana aliumia kichwani.
“Wananchi wanahitaji msaada wa haraka wa Maturubai na Chakula kutokana na kutokuwa na hali mbaya ya kipato cha kukinunua ukizingatia wakati huu ni wa Kilimo, na kwamba madhira hayo yamewakuta wakiwa hawakujiandaa.alisema Diwani Bw. Mwinyi.
Alisema hatua alizochukuwa ni pamoja na kumpigia Karani wa Mbunge wa Mvomero Naibu Waziri Michezo na Utamaduni Bw. Amosi Makala, ambaye aliambiwa anamalizia kIkao na baada ya hapo atawasiliana naye ili kuona njia ya kuwasaidia wananchi hao.
Aidha Diwani Mwinyi alivitaja vitongoji vilivyoathirika kuwa ni pamoja na Chanika nyumba 22, Kibunge 8, Majengo 8, Chongo 7, Mahange 7 na Mikocheni 1, ambapo waathirika wa janga hilo wamehifadhiwa kwa majirani wakati juhudi zna mipango ya kuwahifadhi ikifanywa.
Wilaya ya Mvomero na Kata zake, sehemu hivi karibuni ilikumbwa na ukame ambapo chakula kama Mahindi, Mpunga mazao yanayotegemewa kwa chakula ili kulisha Mkoa na nje, ilikosa Mvua kiasi cha mazao kuathirika na Jua, kwa hiyo mvua hizo zimeanza kwa kasi zikiwa na madhara hayo kiasi kuwafanya wawe na uhitaji mkubwa.
No comments:
Post a Comment