Na Bryceson Mathias, Mvomero
MAJIBU ya waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe kwa Taifa juu ya Hoja ya John Mnyika (Chadema) yamemponza na kuwa mwiba kwa Diwani wa Kata ya Mvomero, Selemani Mwinyi (CCM) kwa wananchi wake, wakimtaka atoe sababu za Mkandarasi wa mradi wa Maji kusimamisha vyombo wakati ulitakiwa ukabidhiwe Januari, 2013.
Akikiri kubanwa na wananchi kuhusu mradi huo hivi karibuni, Selemani alisema ni Kweli Wakandarasi wa Mradi huo unaogharimu zaidi ya Bil. 2/- umesimama bila taarifa ya maelezo ya Msingi ambapo wananchi wamembana wakidai eti wanamtaka Prof. Maghembe wampatie madudu ya mradi huo.
Mapema Januari 15, 2013kabla ya hivi karibuni, wakazi wa Mji mdogo wa Mvomero walimlalamikia Diwani wao kuhusu kusua sua kwa Mradi wao wa Maji kutokana na Wakandaarasi kutolipwa ili kuukamilisha kwa wakati, Lakini baadaya Malumbano ya Maji bungeni, wamemkalia kooni Diwani wao wakimtaka Prof. Maghembe akajibu hoja zao, ili nao waanike madudu ya mradi huo.
“Mradi ulianza Januari 2012 ulitakiwa ukabidhiwe mwaka jana June 6, 2012, lakini sasa umesimama na haujulikanai utaisha lini, hivyo tunalazimika kuoga, kufua na kuchota maji ya kunywa yasiyo salama mtoni, kutokana na miundo mbinu ya awali kufumuliwa” walisema wananchi kwa nyakati tofauti.
Mwandishi alifika eneo la Kazi na kukuta Mkandarasi amesimama kufanya kazi ambapo wafanyakazi waliokuwepo na kuomba wasitajwe kwa sababu si wasemaji walisema, kutokana na kutolipwa kwa wakati wameshindwa kuendelea na kazi.
Mhandishi Mshauri aliyepigiwa simu na kujitaja kuwa ni Steve Mwakangili akiwa safarini kuelekea mwanza alikiri Mkandarasi kusimamissha kazi, alipoulizwa iwapo malipo wamelipwa alisema, anachofahamu tangu Mkandarasi alipolipwa Mil. 600/- hajalipwa tena ingawa kazi imeshafanyika asilimia 88% .
Kampuni inayojenga Mradi huo kwa kusuasua na kulalamikiwa na wananchi wa ni Kampuni ya Kichina (CCECC) ikifanya kazi sambamba na Kampuni ya Ushauri ya Kimisri-AAA-Consulting Engineer, abazo baada ya kuongezewa muda toja June 2012, zilitakiwa kukabidhi Mradi Januari 2013 lakini bado.
Aidha Fununu na Hisia zilizozagaa kwa wananchi zinadai, wakandarasi wanashindwa kulipwa kwa sababu kuna tuhuma Mradi huo ikiwemo ya Maji Turiani wa takribani Bil. 2.7/-, Kilosa Bil. 3/- na Gairo Bil. 7/-, inadaiwa fedha zake huenda zimetumika kwa shughuli nyingine wakidai ni Uchguzi wa 2010 jambo ambalo halijathibitishwa, na kudai inakusudiwa imalizike 2014/2015 ilenge uchaguzi mwingine.
No comments:
Post a Comment