Uongozi wa mtandao huu
umesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa blogs, kuwa
wakiiba kazi za watu katika blogs mbalimbali yaani ‘Kukopi na Kupaste’ kutoka
katika blog Fulani na kuweka katika Blogs zao bila kujali haki miliki ya kazi
ya mtu, wala kumpa haki yule aliyechukuliwa kazi yake kwa kuandika mahala
ulipochukua kazi hiyo.
Kama inavyojulikana
utafutaji wa habari si lelemama na ikumbukwe ili kupata habari iliyo bora na
itakayowafurahisha wasomaji wako, kwenda na wakati ni lazima uihangaikie na
katika kuihangaikia kuna gharama kibao zinazotumika, ikiwa ni pamoja na
usafiri, pesa, na hata mafuta ya gari kutoka mahala Fulani kwenda sehemu
nyingine, gharama za simu na hata kuwalipa wale unaowatuma ili kukufanyia kazi
hiyo.
Kama umeweza kufanya
mambo yote hayo kwa gharama unazozijua wewe uliyeweka stori, ama picha katika
Blog yako, halafu watu wenye Blog Fulani wasio na uwezo wa kufanya kazi na
kuchukua kazi yako kana kwamba ameokota tu jalalani na anaweka kwake ili
wasomaji wake wasome, bila kuwajulisha kuwa kazi hiyo iliyomvutia imefanywa na
mtandao Fulani kwa kweli inaumiza, inaudhi na inarudisha nyuma malengo hasa ya
kuwa na mitandao hii, wote tutajaonekana wapuuzi.
Mtandao huu
umewavumilia watu hawa kiasi cha kutosha lakini sasa imezidi kukithiri, kwani
jamaa hawa wapo katika ukurasa wako kukusubiri kuona tu ulichoweka kwa wakati
huo, ili wao wakopi na kupaste kwao, halafu tayari wamemaliza wala hawataki
kujihangaisha kufanya kazi ili kuboresha mitandao yao na kuwavutia wasomaji
wao.
‘Unapoamua kutangaza
vita ujue tayari umeshajipanga kukabiliana na kila litakalotokea mbele yako, na
pia umejipanga katika kutoka upinzani wa kweli ili watu waone na wakutambue,
lakini sio kwa staili hii ya kuomba mtangaziwe blog zenu kupitia kwa wale
walioanza mapema halafu kumbe kazi yenyewe ni kuchukua kazi za watu tu na si
kufanya kazi’ yaani kukopi na kupaste,
Kuna msanii mmoja
alichoshwa na wenzake wanaotamani kuingia kwenye gemu, lakini wanashindwa
kuumiza vichwa kubuni ili kuweza kupata radha tofauti, na kuamua kuwafikishia
ujumbe kwa kuwaimba kuwa ‘Si lazima wote tuimbe kuna michezo mingi hata kucheza
bao kama huwezi kuimba, ikiwa kila wimbo unaotoka mpya umekopiwa, kama si
mashahiri, basi ni Beat,
Na hata katika
mablogger si lazima wote tuwe na Mablogger, kama huwezi kuumiza kichwa utoke
vipi, basi kaa pembeni waachie wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo, kukopi na
kupaste hadi mitandao yote inakuwa sawa nini maana ya habari za haraka
mtandaoni?,
Huoni kuwa mnawachosha
wasomaji wenu, kwa kosoma habari na picha zinazofafa kwa wakati mmoja na katika
mitandao yote?,
Tena msomaji wako wakiwa
ni waelewa hawawezi kusoma tena mtandao wako kwani habari kama hiyo hiyo walikwishaiona
katika mtandao Fulani muda mchache uliopita na dakika chache baadaye wanaikuta
vile vile walivyoisoma kwingine ikiwa katika ukurasa wako, mara moja mara mbili
msomaji huyo si umempoteza?’’.
Mablogger acheni uvivu
na mjitume msisubiri kukopi na kupaste tu, na kama ukifanya hivyo basi jitahidi
kumpa credit yule uliyemchukulia kazi yake.
VITU muhimu vy kuwa
navyo ili kufanikisha kazi yako ya Blog, ni Laptop ‘Kompyuta mpakato’, ama Desk
Top, Modem ‘Internet Wireless’, Kamera hata ndogo tu ya mkononi, na pia ujue
maana ya kuanzisha hiyoBlog yako na malengo yako kwa jamii, kwani sidhani kama
unaweza kuanzisha blog ili uwe ukisoma mwenyewe na naniliu wako tu.
Na kuwa na kamera si
bora tu kuwa kamera pia ujue kuitumia ipasavyo ili kunasa picha nzuri uitakayo
na itakayofikisha ujumbe kwa wasomaji wako hata kwa kuiangalia tu, kwa kile
ulichokusudia kuwaarifu wasomaji wako.
Baadhi ya Blogs zenye
tabia ya kukopi na kupaste orodha yake tayari tunayo na baada ya tangazo hili, zikiendelea
tutaziweka hewani ili wasomaji wajue ni Blog ipi ya kweli na ipi ni mamluki.
No comments:
Post a Comment