Na Mwanakombo Jumaa- Maelezo, Arusha
Vijana nchini wameshauriwa kuzitumia vizuri fedha za mkopo wa mfuko wa maendeleo ya vijana
ili kuwawezesha kukuza uchumi wao na hivyo kuondokana na
umaskini.
Hatua hii pia itawawesha kukuza kipato chao na hivyo kubadilisha
maisha yao hatua ambayo itasaidia kupunguza tatizo la ajiira nchini kwa makundi
ya vijana.
Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Habari , Vijana ,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara wakati wa ziara yake ya kuvitembelea
vyama vya ushirika wa akiba na mikopo (Saccos) mbalimbali viliv yopata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya
vijana unaosimamiwa na wizara hiyo.
Mfuko huo ambao lengo
lake ni kuwasaidia vijana ama vikundi vya vijana ili waweze kujiajiri kupoitia shughuli za
uzalishaji mali na miradi ya kiuchumi.
Dkt. Mukangara amesema
mikopo inayotolewa na wizara yake
ni jitihada za serikali kuwasaidia vijana na wajasiliamali ili waweze kujikwamua kiuchumi katika maisha, hivyo alisisitiza suala la uaminifu, nidhamu na
uadilifu katika kutumia mikopo hiyo
likiwemo suala la vijana hao kurejesha
kwa wakati mikopo hiyo.
Akiwa katika
kutembelea saccos ya soko kuu waziri Dk. Mukangara alielkezwa na katibu wa
ushirika huo Philipo Kullaya kuwa
ushirika huo una wanachama wapatao 597 ambapo asilimia 70 ni vijana
Alisema ushirika huo
umefanikiw akuwapatia wanachama wake wakiwemo vijana mikopo yenye thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 847.
Aidha alimweleza waziri kuwa saccos hiyo kwa mwaka 2009/2010 ilifanikiw
akupata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wamaendeleo ya vijana
unaosimamiwa na wizara yake ambapo
vijana wapatao 22 walinufaika na fedha
hizo.
Kufuatia hali hiyo
Waziri Dkt. Mukangara amefarijika
kuona wajasirirmali ni kwa jinsi
gani wamenufaika na fedha hizo na jinsi
walivyoweza kurejesha mikopo kwa wakati
Amesema hatua hii
imesaidia kuwawezesha vijana kuwatengenezea ajira za uhakika na pia kutengeneza
ajira kwa vijana wengine mkoani Arusha.
Hata hivyo
wanaushirika hao walimweleza waziri huyo kuwa wanakabiliw ana changamoto
kubwa ya kukosa elimu ya ujasiriamali pamoja na mitaji midogo ili kupanua wigo
kwa vijana wengi kuweza kupata mikopo kutoka
mfuko huo wa maendeleo ya vijana.
Katika ziara yake pia ameziagiza taasisi za wizara yake ikiwemo Idara ya Habari (MAELEZO) , Kampuni ya
magazezi ya Serikali (TSN) na Shirika la
Utangazaji nchini (TBC) zifanye kazi kwa
kushirikiana
Waziri Mukangara amesisitiza kuwa hivi ni vyombo vya
serikali na hivyo vinapaswa kutetea sera za serikali pamoja na kujibu hoja
mbalimbali zinazozoikabili serikali kwani vyombo hivi ndio mdomo wa Serikali.
Katika ziara yake amevitembelea ushirika wa PETU SACCOS, Soko KUU SACCOS pamoja na
Krokon SACCOS ambapo alipata fursa ya
kuongea na viongozi pamoja na wanachama
No comments:
Post a Comment