HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 17, 2013

Extra Bongo yatambulisha nyimbo mbili mpya


DAR ES SALAA, Tanzania 

BENDI ya Muziki wa Dansi hapa nchini, Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ juzi usiku ilitambulisha nyimbo zake mbili Mgeni na Hafidhi katika ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam.

Wimbo wa Mgeni umetungwa na Khadija Kimobitel huku Hafidhi unozungumzia jina la kijana mmoja ukitungwa chini ya mtunzi Athanas Michael.

Nyimbo hizo zilionekana kuwavutia wadau mbalimbali wa muziki huo walioudhulia shoo hiyo, na kujikuta wakiwatuza wanenguaji wa kiume ambao walionyesha shoo ya kuvutia hadi mashabiki kupigwa na butwaa na kushindwa kucheza.

Akizungumzia nyimbo hizo, Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alisema, huu ni mwanzo kwani bendi yake imejipanga ipasavyo kuachia ngoma nyingi kabla ya mwaka hu kumalizika.

“Hizi nyimbo mbili na watunzi tofauti, na lengo kubwa na kuwapa vitu vya tofauti mashabiki wangu, wasiboleke na nawahaidi kuendelea kuwapa burudani mulua zaidi,”alisema Choki.

Nae Shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Husna Abdallah alisema, mwanzoni alikuwa anakwenda bendi mbalimbali ambazo hakutaka kuzitaja na kudai kuwa amevutiwa na Extra bongo jinsi ambavyo wanaimba mpaka wanenguaji walio nao.

No comments:

Post a Comment

Pages