HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 18, 2026

KATELE ACHAGULIWA TENA MWENYEKITI WA TUGHE MKOA WA PWANI

Na Victor  Masangu, Pwani

 

Hatimaye Chama cha wafanyakazi wa serikali na afya  (TUGHE) Mkoa wa Pwani kimefanya uchaguzi wake mkuu na kuweza kumchangua kwa kishindo Mwenyekiti  aliyekuwa anatetea  kiti  chake  Catherine Katele ambaye ameweza kuibuka na ushindi baada ya   kupata kura 33 dhidi ya mpinzani wake ambaye amejinyakulia kura zipatazo 18 kati ya kura halali 51 ambazo zimepigwa.



Katika uchaguzi huo ambao  ulifanyika  katika ukumbi wa Mkuu  wa Mkoa wa Pwani ulihudhuliwa na wajumbe mbali mbali kutoka Wilaya zote saba za Mkoa wa Pwani zikiwemo, Kibaha, Rufuji, Bagamoyo , Mkuranga, Mafia,Kisarawe, pamoja na Kibiti ulikuwa na amani na utulivu katika kipindi chote cha uendeshaji wa  zoezi  zima la upigaji wa kura.  

  

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni  Afisa kazi   Mkoa wa Pwani Metta Nahonyo  amesema kwamba uchaguzi umekwanda vizuri bila ya kuwa na dosari ya aina yoyote na kwamba wagombea wote wamekubalina na matokeo ambayo yametokea na kuongeza kuwa  fomu zote wameweza kuzisahi  bila shaka ya yoyote ikiwa ni ishara tosha ya kuridhika na matokeo hayo.


Msimamizi huyo  amebainisha kwamba katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo Mwenyekiti ambaye ambaye alikuwa anapambana kukitetea kiti chake Catherine Katele ameweza kuibuka mshindi kwa  kupata kura za halali zipatazo 33 huku mpinzani wake Ivo Ndukeki ameweza kupata kura za halali zipatazo 18.

 

"Nikiwa kama msimamizi wa uchaguzi huu wa Tughe Mkoa wa Pwani nimeweza kusimamia vizuri mwenendo mzima wa zoezi hili  la uchaguzi na ninashukuru Mungu kwamba zoezi hili limemalizika salama bila ya kuwa na kosaro ya aina yoyote ile na wagombea wotte wamekubaliana na matokeo ambayo yametokea kwani uchaguzi ulikwenda vizuri  na kila mgombea  ameridhika na ameweza kusaini fomu ,"amebainisha Msimamizi huyo.


Kwa upande wake  Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Pwani ambaye  ndiye alikuwa akitetea kiti hicho kwa mara nyingine amewashukuru kwa dhati wajumbe wote wa Mkutano mkuu wa kuweza kumuanmini kumchagua tena kwa mara nyingine na kwamba ataendelea kuwapa ushirikiano wa hali na mali katika  kukijenga chama bila kuwa na ubaguzi wowote.


Mwenyekiti huyo amesema kwamba kwa sasa mikakti ambayo amejiwekea ni kuweza kuimarisha  nguvu kazi katika sula zima la kuwatetea wafanyakazi katika kulinda maslahi yao na kwamba atakuwa nao bega kwa bega ili kuweza kuleta chachu ya maendelea katika nyanja mabali mbali mbali,


Pia hakusita kuelezea jinsi gani atakavyoweza kuwa na mipango madhubuti ya kuendelea kukiimarisha chama kuanzia ngazi za chini hadi Mkoa ikiwa pamoja na kutafuta fursa za kiuchumi  katika Wilaza zote za Mkoa wa Pwani na kuahidi kuwasaidia watu wenye ulemavu ili waweze kujikomboa.\


Mwenyekiti huyo amemshukuru na kumpa pomgeza Rais wa awamu ya Sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kusimama imara kwa kutenga fedga nyingi ambazo zimeleta matokeo chanya katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo .  


Katibu wa TUGHE Mkoa wa Pwani Jonas Rwegoshora amewapongeza viongozi wote ambao wamemeza kuchaguliwa katika mkutano huo na kwamba ataendelea kushirikiana nao bega kwa bega kwa ajili ya mashali mapana ya chama hicho.


Nao baadhi ya wagombea katika uchaguzi huo wamesema kwamba kwa sasa wataweza tofauti zao pembeni na kuungana kwa pamoja na viongozi wote ambao wamechaguliwa kwa lengo la kudumisha upendo amani na na kuleta chachu ya maendelea kwa maslahi ya watu wote hususan wanachama wa Tughe Mkoa wa Pwani na Taifa kwa ujumla.


 Katika uchaguzi mbali na kumchagua Mwenyekiti wameteuliwa wajumbe wa  nafasi mbali mbali ikiwemo nafasi za wawakilishi wa vijana, wawakilishi wa walemavu, pamoja na wajumbe wengine ambao wataweza kuwakilisha  katika ngazi za  Mkoa na Taifa katika mikutano mbali mbali.

No comments:

Post a Comment

Pages