Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi akisikiliza mawazo ya mmoja wa vijana wajasiriamali mwenye nia ya kukataka kukuza biashara yake na kuifanya kuwa endelevu wakati wa uzinduzi wa Mara Foundation ambao uliotoa fursa ya washiriki kuzungumza na wafanyabiashara waliopiga hatua na wenye uzoefu katika kuendesha biashara zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga akimsikiliza mmoja wa washiriki ambaye ni mjasiriamali anayechipukia aliyetaka kupata uzoefu na mawazo zaidi jinsi ya kuendesha biashara yake.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali akimsikiliza mjasiriamali mdogo mwenye ndoto za kuwa mbunifu wa kimataifa.
Ma-Mentors waliokuja kuzungumza na wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya kuwapa mbinu mbalimbali za kibiashara na kuwaongoza kufikia malengo yao.
Taasisi ya Mara Foundation ilianzishwa na Ashish Thakkar ambaye ndie mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Mara Group.
Ashish alitumia muda wake mwingi katika kutimiza malengo ya Taasisi hiyo kwa kuwa alikuwa na imani na wajasiriamali na kuendeleza biashara ndogo.
Tangu mwaka 2009 Taasisi hiyo ililenga mtazamo wake na imefanya vizuri sana nchini Uganda, Tanzania, Kenya na Nigeria katika muelekeo huo.
Kuanzia mwaka 2013 mikakati ya taasisi ya Mara Foundation inaendelea kukua katika nchi za Kusini mwa Jangwa la sahara huku ikiendelea kuongeza wigo wake katika nchi nyingine duniani.
Mara Foundation inafanya kazi ya kubuni na kukuza uchumi endelevu na kufungua fursa endelevu kwa vijana wamiliki wa biashara za kati kwa kupitia vituo vya uwezeshaji vya Mara Launchpad na Mara Launch Fund.
Pichani juu na chini ni Washiriki na wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kabla ya mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu kuzindua Taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Mara Foundation Tanzania Nina Werner (kulia) akizungumza machache kuhusiana na malengo ya Taasisi yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mh. Dkt. Mary Nagu kuizindua rasmi.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akizungumza wakati kuzindua taasisi ya Mara Foundation ambapo amewataka vijana wajasiriamali kutumia fursa ya taasisi hiyo kujijenga kibiashara
Taasisi ya Mara Foundation yenye makao yake makuu jijini Dubai sasa imejikita katika nchi za Afrika ambazo ni Uganda, Tanzania, Kenya na Nigenia kwa lengo kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuwezeshwa kimuongozo na kuwa wafanyabiashara wakubwa ambao wataweza kutoa ajira kwa watu wengine.
Washiriki na wageni waalikwa wakifurahi jambo wakati mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu akitoa risala kwenye uzinduzi wa Taasisi ya Mara uliofanyika hivi karibuni kwenye jengo la Mayfair Plaza.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akikata utepe kuzindua rasmi taasisi hiyo yenye matawi 28 barani Afrika. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Mara Foundation Nina Werner.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Wageni waalikwa wakishangilia kwa makofi.
MC wa uzinduzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Problem Solved Eric Mutta akimkabidhisha Mjasiriamali mdogo Peter Christopher kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (katikati) atakayekuwa mshauri wake wa kibiashara kwa muda wa miezi sita ijayo.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali (katikati) akimpokea mmoja wa wajasiriamali waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation kwa lengo la kuhakikisha anatimiza malengo yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga (kushoto) akipata picha ya ukumbusho na kijana aliyemchagua kumsaidia kimawazo na kumwongoza kwa muda wa miezi sita ijayo mpaka kufikia lengo lake.
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation uliofanyika hivi karibuni Mayfair Plaza.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) na Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mara Foundation.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha (kulia) na Mkurugenzi wa man Magazine Dismas Massawe (katikati) katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Mara Foundation.
No comments:
Post a Comment