HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 17, 2013

Mwanamke aangua juu ya mti afa alikuwa akichuma mapera

Na  Francis Godwin,Iringa 

Mkazi  wa Mwangata  B katika Manispaa ya Iringa Vumilia Sanga (35) amepoteza maisha  yake   baada ya  kuanguka kutoka juu ya mti  wakati akichuma matunda aina ya mapera nje ya  nyumba yake .

Tukio  hilo  limetokea jioni ya  juzi  majira ya saa 10 baada ya mwanamke  huyo ambae anasadikika  kuwa alikuwa akishumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa.

Wakizungumza na mwandishi  wa habari hizi jana   wakazi  wa eneo hilo  wakiwemo  ndugu  wamedai  kuwa  kabla ya  kifo chake marehemu  alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa na inawezekana  tatizo hilo  lilimkuta akiwa  juu ya mti  huo na hivyo kuanguka na  kuchomwa na mti mgongoni na kutokea  tumboni .

Alisema  mkazi  wa eneo hilo alijitambulisha kwa jina  la Adam Kalinga  kuwa  kutokana na  mwanamke huyo  kuanguka juu ya mti majirani  walijaribu kutaka  kumwokoa ila baada ya  kusogea  walikuta  tayari  utumbo na maini  yakiwa nje na kabla hata ya  kumgusa alikata  roho .

Mwenyekiti  wa serikali ya mtaa huo wa mwangata  B Julius Lwimbo amethibitisha  kutokea kwa  kifo hicho na kuwa  hadi majira ya saa 11.45  jioni  polisi  walikuwa bado hawajafika  eneo la  tukio ili  kuutoa mwili  huo .

Pia mwenyekiti huyo amekiri  kuwa ni kweli  mkazi huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa  kifafa na  kuwa  yawezekana kuanguka kwake kumetokana na tatizo la ugonjwa huo na  kuwa baada ya  kuanguka  toka juu ya mti  aliangukia katika  jiti ambalo lilikuwa limechongoka na ndilo  limemtoa uhai wake .

No comments:

Post a Comment

Pages