HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 11, 2026

TCU Yafungua Dirisha la Udahili 2026/27

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027, litakaloendelea hadi Agosti 10, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa, amesema dirisha hilo lilifunguliwa Julai 1, 2026 na linawahusu waombaji wote wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu nchini.

Prof. Kihampa amewahimiza waombaji kuwasilisha maombi yao mapema ndani ya muda uliotangazwa ili kuepuka usumbufu wa dakika za mwisho.



No comments:

Post a Comment

Pages