HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 17, 2013

POLISI WAZUIA MKUTANO WA CHADEMA ULIOKUWA UFANYIKE LEO

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni limemzuia Diwa wa Kata ya Kimara Pascal Manota (Chadema),  kufanya mkutano wa hadhara kwa madai ya ujio wa Rais siku ya Jmaa tano.

Akizungumza na Habari Mseto Blog jijini Dar es Salam leo, Manota alisema huo ni muendelezo wa jeshi hilo kutumika vibaya zaidi kwa kulinda maslahi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Alisema alimshangaa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kimara, Papalika kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa rais anatarajiwa kutafanya ziara katika eneo hilo siku ya Jumatano ambapako haieleweki ziara hiyo inauhusiano gani na mkutano wa jana.

“Sasa huu ni ubabaishaji na hii inadhihirisha wazi kuwa jeshi hili haliko kwa  kusimamia haki bali lipo kwa ajili ya  kulinda maslahi ya CCM ambapo tunawataka watuache tupambane wenyewe sisi na CCM katika majukwaa ya kisiasa si kuwasaidia”alisema Manota.


Hata hivyo, Manota, alisema eneo la Golani alilokuwa afanyie mkutano liko mbali na kule atakako tembelea Rais, ambako atafanyaa uzinduzi wa daraja ambalo wananchi wanadai kuwa ni bovu kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

“Huu ni mchezo wa CCM kwani wameona nataka kuzungumza na wananchi kuhusu maswala mbalimbali ikiwemo mchakato wa katiba pia kuelezea matumizi ya fedha za maeneleo ya kata hiyo jinsi zinavyotumika vibaya ikiwemo na ujenzi wa daraja hilo”alisema Manota

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Charles Kenyela, kutoa ufafanuzi kuhusu mvutano huo, alisema haamini kama kweli diwani huyo aliandika barua kweli.

Alisema kama angeandika barua hiyo, ni lazima mkuu wa kituo hicho cha Kimara angefikishiwa kopi kwa ajili ya uthibitisho kuwa chama hicho kingekuwa na mkutano.

Kenyela alisema hairuhusiwi mtu yeyote kufanya mkutano bila ya jeshi la polisi kupewa taarifa, ili jeshi hilo liweze kutoa ulizi kwa ajili ya kuzuia vurugu endapo zingetokea.

Hata hivyo, kama wanadai wamechezewa rafu yeye ndiye RPC wanayo haki ya kufikisha taarifa hizo kwake ili wa angalie ni kwa nini imekuwa hivyo na wanaweza kukata rufaa mbele kama hawataridhika na maamuzi yake.

Ni hivi karibuni jeshi hilo lilizuia maandamano na mkutano wa Mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema), kwa madai kuwa maeneo waliokuwa wakitaka kupita kuna ujenzi wa barabara hivyo yangeweza kusababisha foleni na usumbufu kwa watu wengine.

No comments:

Post a Comment

Pages