HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 16, 2013

Ufisadi wa mbolea; Mamia CCM watishia kutimkia Chadema


Na Bryceson Mathias, Lukunguni Mvomero.

TUHUMA za Ufisadi na uchakachuaji wa mifuko ya mbolea 600 ya mwaka 2012 na 2013 ya Kijiji cha Lukunguni, Kata ya Kikeo, Mvomero Morogoro, zimewakasirisha wanachama na viongozi  wa Chama cha Mapinzuzi (CCM), ambapo wamekusanya Kadi kwa Mwenyekiti wao na kutishia kutimkia Chadema.

Hayo yalisemwa Jana na Mwenyekiti Serikali ya Kijiji hicho, Login Mnari, baada ya Mkutano uliohusisha wajumbe 25 wa Serikali ya Kijiji, uliowahoji wenzao 11 waliorubuniwa na Viigogo wa Kata na Wilaya na kufanya Kikao cha Siri kijiji Jirani ili waridhie hadaa kuwa walipokea Mbolea ya 2012/13 wakati si Kweli !.

Mnari alidai wajumbe walioamsha tishio la kutimkia Chadema baada ya kubanwa kwenye kikao na kusaini muhutasi kukiri walirubuniwa na vigogo wa  Kata na Wilaya (na Gazeti kuona sahihi) ni, Mwenyekiti Umoja wa Wanawake wao Viliginia Emili na Katibu CCM Tawi la Lukunguni Octaviani Kupeni.

“Vijana 43 wa (UVCCM) kijijini wamenitupia Kadi, ambapo Mamia wakiwemo wa vijiji vya jirani ambao wamechezewa mchezo mchafu kiasi cha kutumia hata majina ya watu waliokufa kuwa walipokea Vocha za Mbolea (Ninazo); wamekasirishwa na tukio hilo, na sasa wanadai wanatimkia Chadema”. alisema Mnari

Alipoulizwa yeye na Wajumbe 24 wa Serikali ya Kijiji kama wanakiri hawakupokea Vocha za Mbolea 450 za 2012 na Vocha 150 za 2013, wakazi wakitimkia Chadema wao watachukua hatua gani? Alisema, “Kama wataendele kumung’unya maneno, watakaobaki wabaki, lakini tulio wengi tutatimka kuepuka  aibu”.

Alisema, Mbolea hiyo ni Mifuko 150-Urea, 150-DAP, 150 ya Mahindi jumla 450 ya 2012. Nyingine ni Mifuko 50-Urea, 50-Minjingu, 50 (ya Mahindi) jumla 150.

Aidha Mapema Diwani wa Kata ya Kikeo Exavery Msambara alipohojiwa na Mwandishi kuhusu tuhuma ya Mbolea Mifuko 450 (2012) mwaka jana, alikanusha vikali kuhusika na Ubadhirifu huo, ambapo alimtaka mwandishi wazunguke naye kwenye ziara ya vijiji vya Kata, asikie kama anasutwa kuhusu mbolea, jambo ambalo mwandishi aligoma.
 

No comments:

Post a Comment

Pages