MKALI wa mbio fupi duniani, Usain Bolt anaweza kuwa mmoja wa
washiriki wa mbio za Diamond League ambazo ni sehemu ya London 2012 Anniversary
zitakazofanyika Julai, baada ya wakala wa mchezaji huo kufichua "makubaliano
chanya" yamefanyika.
Ni mbio za pili baada ya Olimpiki, kwani Bolt hajawahi
kukimbia nchini Uingereza tangu mwaka 2009 kwa sababu ya sheria ya kodi
inayolazimisha mgawo wa pato lake ama zawadi ya ushindi.
Hata hivyo, msamaha wa makato ya kodi kwa "wanamichezo
wasio wazawa wa Uingereza" katika bajeti mpya imeondoa kikwazo hicho.
Mbio hizo za siku mbili za Diamond League zinatarajia
kufanyika Ijumaa ya Julai 26 na Jumamosi Julai 27, ikifuatiwa na siku ya
matukio ya michezo ya Paralimpiki.
Bolt nyota wa mbio fupi raia wa Marekani mwenye 26,
alishinda dhahabu tatu katika Olimpiki ya kiangazi jijini London mwaka jana, akiweka rekodi katika mbio
za mita 100 na kuwasaidia wenzake kubeba dhahabu ya mita 400 kupokezana vijiti.
Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo inatarajia nyota huyo
atashiriki kwa ufanisi ikiwa ni sehemu yake ya kujiandaa na mbio za ubingwa wa
Dunia zitakazokimbiwa jijini Moscow
wiki mbili baadaye.
"Tuko katika makubaliano chanya ya mazuingumzo, ingawa
bado kuna vitu havijakamilika," alisema wakala wa Bolt, Ricky Simms, kuiambia
BBC Sport.
BBC Sport
No comments:
Post a Comment