KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Martine Shigela akifungua shila la wakereketwa wa umoja wa huo la waendesha Bodaboda wa Melela Kololo. Mvomelo mkoani Morogoro, leo Machi 2, 2013. Wapili kushoto ni Katibu wa UVCCM mkoa wa Morogoro, Jumaane Kitundu na Kulia ni Mjumbe wa Baraza la Vijana Morogoro Abubakar Assenga na Juliana Shonza aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) ambaye amehamia CCM hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigela akimkabidhi kadi ya UVCCM, dereva wa Bioda boda Stanslaus Mdumbwa, katika mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika Kijiji cha Melela, Wilayani Mvomelo mkoa wa Morogoro leo, Machi 2, 2013. Juma ya wanachama wapya 65 wa UVCCM walipewa kadi na Shigela. Wapili kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Jumanne Kitundu.
4. Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) Juliana Shonza ambaye amekihama chama hicho hivi karibuni, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa UVCCM, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashada, Kilombero mkoani Morogoro, jana, Machi Mosi, 2013.
"CCM IMEFANYA MENGI", Mzee wa Juma Jumaa mwenye umri wa miaka 80, akitoa ushuhuda huo, kwenye Mkutano wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashada, Kilombero mkoani Morogoro, jana, Machi Mosi, 2013. Kushoto ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa UVCCM Makao Makuu, Omari Suleiman na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Morogoro, Abubakar Assenga.
6. VIJANA wa hamasa wa UVCCM, wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro, wakihanikiza shamrashamra wakati wa mkutano wa UVCCM uliofanyika Uwanja wa Mashada wilayani humo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martine Shigela akimsaidia kupigangoma, Nyandelo Omari wakati wa mapokezi yake, katika kata ya Melela Mvomelo mkoani Morogoro alipowasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara leo, Machi 2, 2013.
No comments:
Post a Comment