HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 10, 2013

Danganya Toto za Tume, zitagharimu maisha ya Watanzania


Na Bryceson Mathias
 
MAISHA ya Watanzania yataendelea kugharimiwa na Danganya Toto ya Tume mbalimbali zisizo na Majibu na tija, hadi vizazi vitakapomalizika.
 
 
Nisema hivyo kwa maana kwamba, kwa sasa tunahitaji Mungu atuchagulie watu watakaoiongoza Tanzania wenye msimamo wa kusema hawapo tayari kuundiwa, kuletewa na kulazimishwa kupewa danganya toto ya tume nyingi zisizo na majibu na tija.
 
Nimeng’amua kwamba, ukimya wa tume Lukuki zinazoundwa na majibu yake kufichwa au kucheleweshwa, ndizo ambazo zimekuwa zikiendelea kuangamiza Watanzania zikisababishwa na uzembe wa viongozi wa serikali, hata kama majibu ya tume hizoo tayari yako mezani mwao.
 
Katika hali na uzembe kama huo, ndipo tunapowataka wabunge wetu bila kujali itikadi zao, wameunganishe nguvu zao ili kuwaokoa watanzania wanaoteseka na kuangamia kwa uzembe wa kutotoa tu maamuzi ya tume hizo wakati ripoti zake zilishawakilishwa kwa watawala.
 
Swali lanngu ni kwamba, Tangu tume zianze kuundwa ni akina nani waliochukuliwa hatua? Mfano; Kuanzia tume ya MV Bukoba hadi  ya juzi ya matokeo ya kidato cha nne, ieleweke Watanzania sasa tumechoka kuneemesha mifuko ya wajumbe wa tume na kufilisi rasilimali zetu.
 
Watawala siwaombi nataka kujua; hivi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa yaliyogharimu vifo vya nguvu kazi 40 ya watanzania kwenye maafa ya kuanguka kwa jingo la ghorofa 16 bado anaaendelea kubaki ofisini? Kwa nini hajajiuzulu na kuona ameua ndugu zake 40?
 
Kwenye nchi za wenzetu wanakojali maisha ya wananchi wao, mtu mmoja akifa kwa sababu za uzembe kama wa maafa ya ghorofa Waziri husika kama Tibaijuka anapaswa awe amewajibika kiutu kabla ya Rais au vyombo vingine kumwajibisha kwa lazima au maandamano.
 
Lakini viongozi wetu nchini wamenyimwa na kukosa utu kuona wanapofanya kosa au kuhusishwa kwa mitafaruku na majanga, ni wagumu kuwajibika na hawana tabia ya kuiga mienendo myema ya uwajibikaji kama ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa walioamua kuachia ngazi kutokana na uzembe wa watendaji wao.
 
Hadi leo Tanzania, Boti na Meli zimezama na kumaliza watu, Magari yanaendelea kuua, Wawekezaji nao kwa upande wao wameua na kujeruhi watu ovyo kwenye migodi na sehemu za kazi hadi kuharibu kuharibu mali na makazi yao ikiwemo Njaa na Maafa mbalimbali.
Lakini pamoja na uzembe huo, hakuna kiongozi aliyewahi kujiuzulu kwa kuwajibika ila bado wameganda na Viyoyozi ofisini mwao, huku wakila kuku kwa mrija kama hakuna watu waliokufa au kupoteza maisha kwenye uongozi wao!.
 
Kama huko nje Waziri mwenye dhamana anawajibika, iweje sisi leo tuwachekee mawaziri wetu wanapozembea kana kwamba wamefanya sherehe ya kuzaliwa (Birthday) wakati wamesababisha kupoteza maisha ya watu (Nguvu kazi ya Watanzania?”
 
Hata hivyo Jambo lingine linaloniudhi  na kunikera ni hiki kitengo kinachoitwa cha maafa cha Waziri Mkuu kwani kimekuwa kikishughulika kutoa vyakula vya misaada kwenye maafa badala ya kutoa na kutafuta mbinu za kudhibiti yasitokee.  Hapa napo, pawajibike.
 
Makala hii imeandikwa na 
 
0715-933308

No comments:

Post a Comment

Pages