Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akionesha aina mpya ya Smart Phone wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Bando na TTCL na kampeni ya punguzo kubwa la bei ya intaneti uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mauzo TTCL, Kisamba Tambwe. (Picha na Habari Mseto Blog)
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akizindua Huduma ya Bando na TTCL na kampeni ya punguzo kubwa la bei ya intaneti uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Bidhaa TTCL, Issaya Ernest.
KAMPUNI ya
simu Nchini (TTCL) leo imezindua huduma mpya ya
Bando na TTCL itakayomuwezesha
mteja kufaidika na meseji bila kikomo
,kuperuzi intaneti na muda wa maongezi
kwenda mitandao yote kwa bei nafuu.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Kaimu Ofisa Mkuu wa Mauzo Peter Ngota alisema huduma
ya bando na TTCL itamuwezesha mteja pia kutuma meseji bila kikomo kwa bei ya
hadi shilingi mia tano.
Alisema
bando TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za kisasa za smart phones za
kampuni hiyo ambazo zinapatikana katika vituo vyao vya simu kote nchini.
Alisema
kampuni hiyo imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile
internet kwa kampeni ya Basti ikimaanisha peruzi internet zaidi kwa gharama
nafuu.
“Hii ni
punguzo la bei la aina yake , mathalani kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa
kinauzwa shilingi 90,000 sasa
kinauzwa shilingi 25,000 hii ni nafasi
sit u kwa wateja waliopo TTCL kuongeza matumizi kwa gharama nafuu bali hata kwa
wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga
na mtandao wa TTCL,”alisema Ngota.
Alisema
Bando na TTCL na kampeni ya Basti zina
manufaa kkwa mteja ikiwa ni pamoja na huduma ya mobile internate kwa gharama
nafuu,vifurushi vya siku ,wiki na mwezi kulingana na mahitaji ya mteja,mobile
internate yenye ubora na kasi ya juu zaidi,kwa kununua modemu ya shilingi
29,900 utapata 2GB bure kuperuzi intaneti.
Aidha alisema
kua huduma ya bando na TTCL inapatikana pia kwa simu za kisasa za smart phones
na inatoa thamani bora kwa pesa huku
akieleza kua kama kampuni kongwe na mhimili wa mawasiliano nchini inatambua
kuwa na jukumu kubwa la kutoa huduma za mawasiliano kwa wateja kote nchini.
No comments:
Post a Comment