HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 27, 2013

MAKAMU WA RAIS DK BILAL ASHIRIKI HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA TANZANIA METHODIST, MSASANI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, Joseph Mayala, leo Aprili 27 wakati wa hafla ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo. Kulia ni Askofu wa Kanisa hilo, Dk Mathew Byamungu. (Picha Na Ofisi ya Makamu wa Rais - OMR)
 Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya maua kutoka kwa watoto wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani.
 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo Aprili 27 kwa ajili ya kuhudhuria Harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo. 
 Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal, akiwasili katika Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani.
 Baadhi ya waumini Kanisa la Tanzania Methodist, Msasani, waliohudhuria Harambee hiyo.
 Juu na Chini: Watoto wa Kwaya inayofadhiliwa na Shirika la Compassion International Tanzania, wakitoa burudani moja ya wimbo wao ulio katika Albam yao iliyozinduliwa katika hafla hiyo.
 Askofu wa Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, Dk Mathew Byamungu, akitoa neno la shukrani baada ya hafla hiyo.
 Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya Wachungaji na Watumishi wa Kanisa hilo.
 Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na watoto wanaounda kundi la Kwaya ya watoto, inayofadhiliwa na Shirika hilo.
Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Watoto.

No comments:

Post a Comment

Pages