HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 11, 2013

MATUKIO MBALIMBALI YA SHUGHULI ZA KIJAMII JIJINI DAR ES SALAAM


 Moja ya jengo zuri la kisasa liliopo katika muungano wa  barabara ya mtaa wa Bibi Titi na mtaa wa  Ohio jijini Dar es salaam linaitwa UHURU HEIGHTS.
  Hivi karibuni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uingereza nchini  imewapatia mafunzo ya  kuwajengea uwezo Maafisa  Mawasiliano kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali jinsi  ya kutumia mitandao ya kijamii katika kuimarisha mawasiliano. Mafunzo hayo yameendeshwa na  Taasisi ya Thomson Foundation na kugharamiwa na Serikali ya Uingereza. Pichani  Mkufunzi wa Mafunzo David Wiggins (katikati) akifurahia zawadi ya shati la kitenge baada ya kukabidhiwa na Afisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi  Judith Mhina (kushoto ) kwaniaba ya wenzake, (kulia) ni Mkurugenzi  wa Idara ya Habari Assah Mwambene.
 Ujenzi wa upanuzi wa  barabara wa mwendo kasi katika ya barabara ya  Morogoro  ukiendelea katika eneo la Magomeni Mapipa, ujenzi huo utakapomalizika utarahisisha usafiri katika jiji la Dar es Salaam na kupunguza msongamano wa magari.
 Maafisa Mawasiliano Serikalini wakiwa katika picha ya pamoja. baada ya kumaliza  mafunzo ya  jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii  kama facebook,twitter, flickr nablogs. 
 Mkufunzi kutoka  Uiengereza David Wiggins akiwaaga Maafisa Mawasiliano Serikalini (hawapo pichani) baada ya kumaliza  mafunzo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) 
Ujasiramali upo wa aina nyingi ili kujisaidia katika kupata kipato na kuweza kujikimu . Pichani  kijana akiwa amejiajiri kwa kazi ya kufuta vioo vya magari katika eneo la barabara ya Morocco jijini Dar es Salaam kama kamera yangu ilivyomnasa hivi karibuni. 

No comments:

Post a Comment

Pages