NA EDITHA WILLIAM, KAGERA
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Dkt. Peter Mkenda amehamasisha wananchi kupima magonjwa ya afya ya akili katika vituo mbalimbali vya afya vilivyopo ndani ya Mkoa wa Kagera
Dkt. Mkenda ametoa kauli hiyo akiwa ofisini kwake ikiwa ni ya siku chache baada ya serikali kupitia wizara ya afya nchini kuhamasisha wananchi kutekeleza afua mbalimbali za afya ikiwemo kupima matatizo ya afya ya akili
"Ni changamoto kubwa ambayo imekuwa katika jamii na kwa kiasi kikubwa watu hawana ufahamu wa kutosha juu ya magonjwa ya afya ya akili".
Aidha amesema kuwa afya ya akili inatokana na msongo wa mawazo, wasi wasi uliopitiliza, hisia {kutokuwa na uhalisia wa jambo} pamoja na matendo ya mtu kubadilika kuwa kwenye mfumo tofauti na jamii ilivyomzoea.
Vilevile, Dkt Mkenda ameshauri wanajamii kuwa wawashirikishe watu wa karibu pamoja na wataalamu wa masuala ya saikokolojia pale wanapokuwa na msongo wa mawazo au jambo linalohitaji msaada wa mawazo ya mtu mwingine ili kuepuka kuathirika kisycholojia wakati mwingine kujichukulia sheria mkononi.
"Shida kubwa ya ugonjwa wa akili mgonjwa mwenyewe anakuwa hajui na wakati mwingine uwa wakimya na kushindwa kushirikisha mawazo yao watu wa karibu kama familia, marafiki, au jamii mara nyingi mtu anajiamulia na kuchukua maamuzi magumu kama kujinga'.
Ikumbukwe kuwa Mei 11, 2026 Waziri wa Afya Mh. Mohamed Mchengerwa wakati akiwasilisha bajeti ya wizara ya afya kwa mwaka wa fedha 2026/ 2027 bungeni jijini dodoma aliwasihi wananchi kote nchini kupima matatizo ya afya ya akili katika vituo vya kutolea huduma za afya na kusema kuwa matatizo ya afya ya akili yanatibika endapo yatagundulika mapema
" Nitoe rai kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya kupima magonjwa ya afya ya akili hususani msongo wa mawazo na sonona" alisema Waziri Mchengerwa.





No comments:
Post a Comment