HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 07, 2013

Sh. 125, 000 ZAMUENGUA MWENYEKITI CCM


Na Bryceson Mathias,
 
SHILINGI 80,000/- Elfu zikiwa ni gharama za Matofali 800 (kila moja Sh. 100/-), na Sh. 45,000/- zikiwa ni michango ya wana kijiji wa Mafuta, ndizo zilizoelezwa kuwa kigezo cha kumuengua Uenyekiti wa Serikali ya Kijiji Bw. Waziri Juma toka mwaka jana.
 
Hayo yamebainika jana baada ya Mwandishi wa Habari hizi kufuatilia kujua nini kinacholeta vurugu na Migogoro ndani ya Serikali ya kijiji hicho ambapo sasa wananchi wanatishia kukataa kufanya kazi zote na Mtendaji Kata ya Mhonda Bw. Emili Mjenja.
 
Akizungumzia Mtafaruku huo Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji Bw. Jafari Seleman mjumbe alikiri kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi kati yaa baadhi ya Viongozi wa Kata na wale wa kijiji hicho ambapo alisema, kumekuwa hakuna Ueledi katika Mapato na matumizi ya Michango yao.
 
“Si jambo la Siri kumekuwa hakuna mahusiano mema kati ya Viongozi wa Kata na wananchi wa Kijiji cha Mafuta, ambapo wanasema viongozi wa kijiji wanashirikiana na wa Kata kwa namna fulani, kuhujumu Mali, Michango na Mapato ya Kijiji, ndio maana wamemkataa Mwenyekiti”. Alisema Selemani.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa sasa Bw. Nicholous Mbelwa aliyechaguliwa na wananchi baada ya kuangushwa Bw. Juma aliwalaum viongozi wa Kata akiwatuhumu kuwa wanafanya mchezo na Masha ya Wananchi ambao wanateseka kuokoa kuokoa nguvu na juhudi za serikali.
 
Aidha Diwani wa Kata ya Mhonda Bw. Salum Mzugi (CCM) alipoongea na mwandishi wa habari hizi alisema, anasikitishwa kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara inayohusu upinzani wa vyama kwa sababu inawaondolea wananchi maendeleo waliokusudia, ambapo aliahidi kuyapatia  ufumbuzi wa kina.
 
Kiti cha mwenyekiti wa Kijiji hicho, kimekuwa na Mvutano toka mwaka jana Julai 7, 2012, ambapo wanakijiji walimng’oa Mwenyekiti Juma kwa tuhuma za ubadhirifu na madai ya kukwamisha maendeleo ya wananchi, ambapo Mtendaji Kata Bw. Mjenja anatetea asiendelee, huku wananchi wakigpinga.

No comments:

Post a Comment

Pages