HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2013

Spika Makinda: Fedha ya Umma isichezewe kwa vikao Batili


 Na Bryceson Mathias

HIVI karibuni Spika Anne Makinda aliitaka Kamati ya Kanuni kukutana kwa dharura kujadili ukiukwaji wa kanuni mpya walizojiwekea, na hivyo kufikia hatua ya wabunge kujadili jambo lililoko mahakamani.
Mshangao wangu ni kwamba, Spika Makinda alikuwemo bungeni huku akishuhudia Wabunge wake wakivunja sheria huku mwenyewe wengine akiwaruhusu na wengine akiwanyima nafasi ya kuchangia kutokana na Lungu na sababu alizonazo mwenyewe.
Haihitaji kwenda Eckenford Tanga kupata ushauri nasaha wa kuwazuia wabunge bungeni wanapokosea Kanuni ambazo Bunge limejiwekea. Tataizo ni pale kiongozi unapokuwa sehemu ya kuvunja Kanuni hizo hapo ndipo huwa umejifungia na huwezi kusema ukaheshimiwa.
Makinda na yeyote atakayekaa kwenye kiti cha U-Spika, kamwe hatatenda haki na kufuata Kanuni za Bunge inavyopaswa kama ataendelea kuchaguliwa kutoka ndani ya Vyama tena kwa mizengwe ya Hila na Upendeleo wa mashinikizo. Lazima Spika asiwe Mbunge na asitoke Chama cha aina yoyote.
Kosa kubwa la Spika Makinda na Naibu waka Job Ndugai; wakikaa kwenye kiti hicho kutuwakilisha watanzania, huwa wanasahau kama wanawatumikia wananchi Milioni 14 wenye Vyama na wasio na Vyama, badala yake wanaona wanawatumikia wananchi wa Itikadi yao.
Kimsingi Wandishi tumechoka kurudia rudia kusema; maana kila tunapozungumzia ukiukwaji na kudorora kwa utu wa kiti cha Spika katika kutenda haki, tunajisikia kama tunampigia Mbuzi Gitaa asiyesikia wala kutotaka kubadilika katika wakati huu wa kukua Demokrasia kimataifa.
Bado sielewi kwa nini Kiti cha Spika bado kiko enzi ya Adamu Hawa badala ya kuingia Digitali ambayo nayo imekumbwa na ukiritimba wa kuiga usio na maono ya maandalizi halisi ambayo, hadi sasa badala ya kuwapa raha watanzania, yanawapa kero.
Mhe. Makinda; hakukuwa na sababu za Msingi, kuwaachia wabunge wajadili hoja kwa kukiuka Kanuni zenu za Bunge  huku ukiwaruhusu mwenyewe, halafu baadaye useme Kamati ya Kanununi ikutane kwa dharura. Licha ya kwamba muda wa tafakuri kwa wabunge kupembua mambo mengine, unapotezwa pasi na sababu.
Mbali ya hilo, kama kuna vinywaji baridi, Vitafunio, vitatumika katika vikao vya namna hiyo; basi gharama ya ununuzi huo ambayo Kodi ya walalahoi, inapotea pasipokuwa na sababu, kwa sababu kujadili suala hilo hakukuwa na msingi gharama yakke ilikuwa ndogo tu, ambayo nikutumia Mamlaka ya  Spika kupinga ukiukwaji huo bila kuisumbua Kamati.
Wakinga wana Msemo wa maonyo haya!  Kama ulimuona mwizi akiingia Shambani ..akavunja mahindi unamuona, akaanza kutoka nayo shambani unamuona, ina maana umemruhusu afanye alichofanya;  hivyo ukianza kulalamika, huna sababu ya kupiga kelele.
Vivyo hivyo kwa Spika Makinda, Wabunge walipokuwa wanaomba kuzungumza uliwaruhusu, walipoanza kukiuka Kanuni uliwasikia, na wengine walipoomba mwongozo uliwaruhusu, nao walipoendeleza kukiuka, uliwaruhusu!! Sasa unataka kikao cha Kamati ya Kanuni, ya nini wakati uliruhusu mwenyewe?.
Kwa hilo, Spika unawatia majaribuni Wana Kamati, lakini pia unapunguzia ueledi wao kwa wananchi wanaowafahamu, konekana kuwa  wanajadili hata mambo yasiyo na tija, na hivyo kuonekana wanaweza kuburuzwa hata penye ubovu badala ya mambo ya uchanya wa hoja.
Napata Tabu sana kama itafikia wananchi watabaini Bunge halijadili vitu kwa kujali matumizi mazuri ya gharama za uendeshaji wa vikao mbalimbali kwa kodi ya wananchi. Ni lazima tusikie maumivu yake, yu mkini yafanyike mambo ya msingi kuliko kukurupuka.
0715933308

No comments:

Post a Comment

Pages