HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 26, 2013

Uwekaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Kivuko cha Dsm- Bagamoyo


 Kivuko cha Dar- Bagamoya. Picha na Mwanakombo Jumaa Maelezo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa (kulia) akizungumza  katika hafla ya uwekaji saini  mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini. Kivuko hicho  kitakuwa na uwezo wa  kubeba watu 300 , kitagharimu  shilingi7.91 bilioni. (bilioni7.91 za tz).Pichani  kutoka kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dkt,John Magufuli,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mecky Sadick, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Balozi Herbert Mrango.
 Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Marceline Magesa (wa pili kulia), na Mwakilishi wa Kampuni ya,  Johs Gram Hanssen A/S ya  Denmark,  Andreas Gottrup wakiweka  saini mkataba wa ujenzi wa Kivuko  cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyoshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (aliesimama katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick(alie vaa  shati la kitenge) Balozi wa Denmark nchini Tanzania  Mh, Johnny Flinto (mzungu aliesimama  mstari wa nyuma). Pamoja na watendaji wakuu wa  Wizara ya Ujenzi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Mecky akizungumza wakati wa  hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa  Kivuko cha Dar es salaam – Bagamoyo. Kivuko hicho kitagharimu shilingi 7.91 bilioni za kitanzania. Mwengine ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Pages