Na Bryceson Mathias, Mafuta – Mhonda Morogoro
WANANCHI wa Kijiji cha Mafuta Kata ya Mhonda Wilayani Mvomero, wamemlalakia Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba, wakidai Uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba umevurugwa na Watendaj wa Vijiji na Kata.
Hayo yamesemwa na kuungwa mkono na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mafuta wakati Waandishi wakitembelea vijijii kuhakiki jinsi chaguzi hizo zinavyoendeshwa, huku watu wakdai hawajaona matangazo wala taarifa zozote, ila wanasikia kuna watu wamepewa Fomu kinyemela.
Akizungumza na waandishi wa habari, Bw. Nicholous Mbelwa ambaye ni Kaimu Mwenyekiti aliyechaguliwa na Wananchi baada ya kumkataa Bw. Waziri Juma anayetuhumiwa kufuja fedha za wanakijiji mapema Julai 16, 2012 alisema,
“Hatujui Uchaguzi huo utafanyika lini kwa sababu, hakuna matangazo yanayoelekeza kuomba na kujaza fomu kuchaguliwa kwa wajumbe hao na Majina yao kubandikwa kwenye mbao za matangazo kama sheria ilivyoekeza.
“Ila kuna fununu kwamba kigogo mmoja wa Kata amewapa watu wanne (4) fomu za maombi ya ujumbe huo kinyemela ili wajaze bila kuwepo Mkutano Maalum, na kwamba kuna Mtu amepewa fomu yeye na Mke wake, hivyo tunasubiri kitaeleweka”.alisema.
kijiji cha Mafuta kipo mbele ya vijiji vya Magole na Hubiri, ambapo uelewa Mdogo wa Elimu Uchaguzi huo kwa wananchi umetumika kama nafasi ya kuvuruga taratibu za Tume ya Katiba katika kufikia azma sahihi ya Sheria ya kupata wajumbe wa Mabaraza hayo.
Aidha Mwandishi alipomtafuta Elimily Mjenja kwa simu ya Mkononi ili kujibu tuhuma hizo bila mafanikio, lakini ilimpata Diwani wa Kata ya Mhonda Bw. Salum Mzugi, aliyekanusha Kigogo yeyote wa Kata kugawa Holela fomu hizo bila kufuata utaratibu ulioelekezwa.
“Yanatakiwa yapita matangazo ya kuwataka wananchi wachukue fomu waombe kuchaguliwa,majina ya wagombea yabandikwe katika mbao za matangazo, na hatimaye uitishwe Mkutano wa hadhara au Mkutano Maalum kuwachagua. Kama hali hiyo, ipo Nitaishughulikia”.
Mapema wananchi walirusha Tuhuma kwa vigogo wa Kata akiwemo Diwani Bw. Mzugi, Mtendaji Kata Mjenja na Mtendaji wa Kijiji aliyejulikana kwa Jina moja Bw. Mahunda kuwa wanavurunda taratibu za Uchaguzi wa Mabarza ya Katiba, Jambo walilolipinga.
No comments:
Post a Comment