Na Elizabeth John
MSANII nyota wa miondoko ya hip hop,
Sharifu Thabiti ‘Darasa’ amepanga kuwa na utaratibu rasmi wa kuuza albamu yake
ya kwanza ambayo iko katika hatua za mwisho kukamilika.
Akizungumza na Habari Mseto, Dar es Salaam juzi, Darasa
alisema kwa sasa anaandaa michakato hiyo kuepuka ubabaishaji katika soko la
muziki nchini ambalo linapunguza maslahi katika kazi za sanaa hiyo.
“Sihofu changamoto zilizopo sokoni
katika usambazaji albamu kwani najipanga kwa lengo la kukupambana ili
kuhakikisha nafanya vizuri na kuweka historia nyingine,” alisema Darasa.
Alisema
kwa vile msanii kamili, ni lazima awe na albamu sokoni kwa heshima na
hadhi yake katika jamii, basi kazi zake ni muhimu kuwa na hadhi inayostahili
kulingana na ubora wake sokoni.
Aliongeza kuwa albamu yake inatakuwa na
nyimbo 14 huku ikitarajiwa kuingia sokoni wakati wowote kuanzia sasa baada ya
mchakato kukamilika.
No comments:
Post a Comment